Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Slaa, Rais Magufuli wateta Ikulu
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa, Rais Magufuli wateta Ikulu

Spread the love

BALOZI wa Tanzania nchini Sweden, Dk. Willibroad Slaa, amerejea jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na Rais John Pombe Magufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Haikuweza kufahamika mara moja, kilichojadiliwa katika mazungumzo kati ya Dk. Slaa na Rais Magufuli.

Hata hivyo, katika siku za karibuni iliripotiwa kwenye vyombo vya habari vya Magharibi na mitandao ya kijamii, kuwa balozi huyo anayehudumu kwenye nchi za Sweden na Finland ameitwa Ikulu ya Sweden “kufokewa” kufuatia hatua ya nchi yake kutoheshimu haki za binadamu.

Dk. Slaa ambaye alikuwa katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), hadi Agosti mwaka 2015, aliteuliwa kuwa balozi na Rais Magufuli katikati ya mwaka huu.

Rais Magufuli alimteuwa Dk. Slaa kuwa balozi, kipindi ambacho alikuwa akiishi “uhamishoni” nchini Canada.

Dk. Slaa alipelekwa “uhamishoni” nchini Canada na aliyekuwa mchumba wake, Josephine Mushumbuzi.

Kwa sasa, taarifa zinasema, wapenzi hao wawili – Dk. Slaa na Josephine – tayari wamefunga ndoa kwenye kanisa moja nje ya nchi.

Josephine alichukua uamuzi wa kumpeleka uhamishoni Dk. Slaa, kufuatia kushindwa kwa mpango wake wa kumng’ang’aniza kuwa mgombea urais wa Chadema/ Ukawa kwenye uchaguzi mkuu wa 25 Oktoba 2015.

Dk. Slaa ambaye ni amewahi kuwa Padri wa Kanisa Katoliki na kuhudumu kwenye nafasi ya Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu la Tanzania (TEC), alikuwa mmoja wa wanasiasa wenye ushawishi mkubwa nchini.

Mbali na kuwahi kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, amepata kuwa mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfululizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the loveCHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!