Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Slaa asema hana chama “nikialikwa CCM, ACT, CHADEMA nitakwenda”
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa asema hana chama “nikialikwa CCM, ACT, CHADEMA nitakwenda”

Balozi, Dk. Willbroad Slaa
Spread the love

 

BAADA ya kuibua mjadala kufuatia hatua yake ya kuhutubia mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mkoani Arusha, Balozi Dk. Wilbroad Slaa, amesema hana chama. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Balozi Slaa ametoa kauli hiyo leo tarehe 28 Februari 2023, akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha Azam, baada ya baadhi ya watu kudai kwamba yuko mbioni kurejea Chadema, alikojivua uanachama miaka minane iliyopita.

Mwanasiasa huyo ameeleza kuwa, yeye hana chama na kwamba hata vyama vingine vya siasa vikimualika kushiriki katika matukio yao yuko tayari kwenda.

“Kwa sasa sina chama, nikialikwa na Chadema nitakwenda na kuzungumza, nikialikwa na CCM pamoja na ACT Wazalendo nitakwenda pia na nitazungumza ,mimi ni Mtanzania ninayejua haki zangu za kisheria na kikatiba,” amesema Balozi Slaa.

Mjadala wa Balozi Slaa kurejea Chadema ulishika Kasi kufuatia ahadi yake ya kutaka kushirikiana na chama hicho katika kudai upatikanaji wa katiba mpya, pamoja nakukikosoa Chama Cha Mapinduzi (CCM), hadharani kwamba kimeshindwa kuongoza nchi.

Mbali na kushiriki mkutano huo wa Chadema uliofanyika Karatu, mkoani Arusha, katika siku za karibuni Balozi Slaa amekuwa akishiriki matukio mbalimbali yanayoandaliwa na Chadema, hususa mikutano ya kidigitali inayofanyika kupitia mitandao ya Club House na Twitter Space, ambapo amekuwa akichangia mada kuhusu masuala ya kisiasa na mchakato wa katiba mpya.

Kabla ya kuachana na siasa hai mwaka 2015, Balozi Slaa alikuwa Katibu Mkuu wa Chadema, ambapo aliamua kujivua uanachama wa chama hicho kufuatia hatua ya chama chake kumpokea Edward Lowassa aliyetokea CCM na kuwa mgombea wake urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!