January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Slaa arejea kwa kishindo

Dr. Willibrod Slaa (katikati) – Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akizungumza na wanachama wa chama hicho, mara baa ya kurejea kutoka nchini Marekani kwa ziara ya siku 10.

Spread the love

DAKTARI Willibrod Slaa – Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amesema uandikishaji wapiga kura kwa mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR) ni mchezo wa kisanii. Anaandika pendo Omary.(endelea).

Mfumo huu unatumika kuchukua au kupima taarifa za mtu za kibaiolojia au tabia za mwanadamu na kuzihifadhi katika kazidata (database) kwa ajili ya utambuzi.

Dk. Slaa ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kurejea kutoka nchini Marekani alikokwenda kwa ziara ya siku 10 akiwa ameongoza na mkewe Josephine Mshumbusi.

“Mchezo wote wa BVR ni usanii. Nimetoka Marekani, huko wana umeme saa 24. Wana huduma ya simu saa 24. Lakini hawatumii mfumo wa BVR katika chaguzi zao,” amesema Dk. Slaa.

Aidha, amesema “Taarifa ya Mtaalam kutoka Marekani ni kwamba, BVR inaashiria yanayofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ni ya makusudi. Inajua kuna wananchi hawataandikishwa. Ndio maana wameanza uandikishaji katika ngome za Chama cha Mapinduzi (CCM).

Dk. Slaa ameongeza kuwa, mbali na BVR kuwa mchezo wa kuingiza, pia ni ufisadi ambao umegharimu mabilioni ya fedha za walipa kodi.

“Tenda ya BVR ilikataliwa na Mamlaka ya Kusimamia Manunuzi ya Umma (PPRA). Hakuna mchakato wowote wa wazi wa zaburi uliofanyika,” amesema.

Akiwa nchini Marekani, Dk. Slaa ameweza kuzungumza na wawekezaji ambao wako tayari kushirikiana na Tanzania. Hatua hiyo ni katika kukuza uchumi wa Taifa utakaonufaisha maisha ya Watanzania.

“Wenzetu wako tayari kushirikiana na sisi. Wapo tayari kuwekeza kwa masharti yetu. Chadema haina ugomvi na wawekezaji. Lakini hatuhitaji wawekezaji wezi, mafisadi na wanaoingia mikataba ya siri na serikali. Hatuko tayari kuona mtu anakuja anachota rasilimali zetu,” amesema Dk. Slaa.

Katika ziara hiyo, pia ametembelea miradi kadhaa ikiwemo ya ufugaji wa ng’ombe wa maziwa na miradi inayoendeshwa na vyuo vikuu ambapo amesema Tanzania inahitaji teknolojia, nyezo za kazi na ujuzi ili iweze kupiga hatua katika maendeleo.

error: Content is protected !!