February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Shika aendelea kusota, Polisi kumpima akili

Spread the love

KAIMU Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Benedict Kitalika amesema jeshi la polisi linaendelea kummshikilia Dk. Louis Shika kwa kuwa bado linaendelea na uchunguzi huku wakijipanga kumfanyia vipimo vya akili, anaandika Angel Willium.

Kitalika amesema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani muda wowote baada ya uchunguzi kukamilika, lakini hadi sasa hakuna ndugu yake yeyote aliyejitokeza kushirikiana na jeshi la polisi katika uchunguzi unaoendelea.

Kamanda amesema kabla ya kumfikisha mahakamani jeshi la polisi linawasiliana na mamlaka nyingine za serikali kuangalia kama kuna uwezekano wa kumpima Dk. Shika kama ana matatizo ya akili.

Dk Shika anatuhumiwa kwa kuvuruga mnada wa nyumba za bilionea Said Lugumi ulioendeshwa na kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart baada ya kushindwa kulipa asilimia 25 ya malipo ya awali ya gharama za nyumba hizo.

error: Content is protected !!