September 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Shein ‘amfuata’ Magufuli Baraza la Mawaziri

Spread the love

RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein leo ametangaza baraza lake jipya la mawaziri ambapo amepunguza kutoka wizara 16 na kuwa 13, anaandika Faki Sosi.

Hatua ya Dk. Shein kupunguza wizara inakenda sambamba na ile ya Rais John Magufuli ambaye alipunguza wizara hizo kutoka 30 za mtanguli wake Rais Jakaya Kikwete na kuwa 19.

Dk. Shein ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar ametangaza baraza hilo ili kumsaidia kusimamia kazi za serikali kwa kipindi cha uongozi wake wake.

Akitangaza baraza hilo amesema, amepunguza ukubwa wa baraza hilo kwa kuvunja wizara tatu na kuzigawa ndani ya wizara 13 za sasa ambapo mawaziri ni 13 na manaibu waziri saba.

Mawaziri hao wantarajiwa kuapishwa kesho Jumapili asubuhi katika Viwanja vya Ikulu visiwani Zanzibar. Mawaziri hao ni;

Issa Haji Ussi Gavu, Ofisi ya Rais na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi; Haroun Ali Sleiman, Katiba na Sheria Utumishi wa Umma; Haji Omari Kheir, Tawala za Mikoa na Idara maalum; Mohamed Aboud, Makamu wa pili wa Rais.

Wengine ni Dk. Khalid Salum Mohamed, Waziri wa Fedha na Mipango; Mahmoud Thabit Kombo, Afya; Riziki Pembe Juma, Wizara ya Elimu; Amina Salum Ali, Viwanda na Masoko; Ali Karume, Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi.

Wengine ni Rashid Ali Juma, Habari Utalii Utamaduni na Michezo; Hamad Rashid Mohamed, Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi; Mauldine Castiko, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto na Salama Aboud Talib, Maji Ardhi Nishati na Mazingira.

error: Content is protected !!