Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Shein afuata nyayo za Rais Magufuli
Habari za Siasa

Dk. Shein afuata nyayo za Rais Magufuli

Spread the love

DAKTARI Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar leo tarehe 11 Juni 2019 amefanya uteuzi wa viongozi katika idara mbalimbali zilizoko chini ya wizara nne. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Katika Wizara ya Biashara na Viwanda, Rais Shein amemteua Juma Hassan Reli kuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, huku Abdulla Rashid Abdulla akimteua kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Viwanda, wakati Ali Suleiman Abeid akimteua kuwa Ofisa Mdhamini wa Wizara ya Biashara na Viwanda Pemba.

Rais Shein amefanya mabadiliko hayo ikiwa ni siku chache zimepita, tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli kufanya mabadiliko katika Wizara ya Viwanda na Biashara, kwa kutengua uteuzi wa aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Joseph Kakunda, ambapo alimteua Innocent Bashungwa kushika wadhifa huo.

Pia, Rais Magufuli alimuhamisha aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Edwin Mhede na kumpeleka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwa Kamishna Mkuu wa mamlaka hiyo, akichukua nafasi ya Charles Kichere aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala mkoani Njombe.

Hata hivyo, Rais Magufuli hadi sasa hajamteua katibu mkuu mpya wa Wizara ya Viwanda na Biashara.

Katika uteuzi wake wa leo, kwa upande wa Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Rais Shein amemteua Dkt.Haji Salim Khamis kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Pia, Rais Shein amemteua Kapteni Khatib Khamis Mwadini kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete na Abeid Juma Ali amemteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A

Naye Saleh Mohamed Juma ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mjini/ Magharibi, na Said Haji Mrisho ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya Magharibi A.

Wakati huo huo, Rais Shein amemteua Yahya Idris Abdulwakil kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Huduma za Maktaba na Dk. Ali Ussi Makame amemteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mkaguzi Mkuu wa Elimu.

Katika Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale, Rais Shein amemteua Chande Omar Omar kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC) wakati Imane Osmond Duwe akimteua kuwa Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar.

Hali kadhalika, Rais Shein amemteua Mwita Mgeni Mwita kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, na Dk.Rahma Salim Mahfoudh amemteua kuwa Kamishna wa Idara ya Ukuzaji wa Uchumi na Mashirikiano baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi.

Vile vile, Rais Shwin amemteua Maryam Nassor Uki kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi katika Tume ya Mipango.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Jaji Biswalo aendelea kung’ang’aniwa fedha za ‘Plea Bargaining’, CUF wataka ajiuzulu

Spread the love  CHAMA cha Wananchi (CUF), kimemtaka aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka...

Habari za Siasa

Bunge labaini madudu mfumo ukusanyaji mapato, h’shauri tatu kikaangoni

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali...

Habari za Siasa

Mkuu wa wilaya ya Rungwe azindua vyumba sita vya madarasa vya thamani ya 64 mil

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amezindua vyumba...

Habari za Siasa

Mbunge afurahia mabilioni ya Samia kutua jimboni

Spread the love  MBUNGE wa Igunga, Nicholas Ngassa ameishukuru Serikali kwa utekelezaji...

error: Content is protected !!