May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Samizi akumbusha ahadi ya Hayati Magufuli bungeni

Hayati John Magufuli

Spread the love

 

MBUNGE wa Muhambwe mkoani Kigoma (CCM), Dk. Florence Samizi, ameihoji Serikali lini itatekeleza ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Afya, cha Kata ya Murungu jimboni humo, iliyotolewa na Hayati John Magufuli, akiwa Rais wa Tanzania. Anaripoti Glory Massamu, TUDARCo … (endelea).

Dk. Samizi amehoji hayo leo Alhamisi, tarehe 2 Septemba 2021, katika kipindi cha maswali na majibu, bungeni jijini Dodoma.

Akiuliza swali hilo, Dk. Samizi amesema, Magufuli alitoa ahadi ya kujenga kituo hicho, ili kusogeza karibu huduma za afya kwa wananchi.

‘’Je ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya Hayati Dk. Magufuli, Makamu wa Rais wa sasa (Dk. Phillip Mpango) na Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa), ya Kujenga Kituo cha Afya Kata ya Murungu, katika Wilaya ya Kibondo, ili kusogeza huduma na kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya?”ameuliza Dk. Samizi.

Magufuli alikuwa Rais wa Tanzania wa awamu ya tano, ambaye alifariki dunia akiwa madarakani, tarehe 17 Machi 2021 na mwili wake kuzikwa nyumbani kwao Chato, mkoani Geita.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Dk. Festo Dugange

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dk. Festo Dugange, amesema Serikali imepeleka Sh.250 milioni, kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho.

“Katika kutekeleza mkakati huu, Serikali imepeleka fedha Sh.25.5 bilioni kwa ajili ya kuanza ujenzi wa vituo vya afya kwenye tarafa 90, zisizo na vituo vya afya ikiwemo Tarafa ya Kibondo Mjini inayoundwa na Kata tisa (9) za Murungu, Bunyambo, Kibondo Mjini, Biturana,” amesema Dk. Dugange na kuongeza:

“Kumwambu, Kitahana, Rusohoko, Misezero na Bitare ambapo kiasi cha Sh. 250 milioni kimepelekwa kwa jili ya ujenzi wa Kituo cha Afya, kwenye Kata ya Bunyambo.”

error: Content is protected !!