Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Samia ateua viongozi 6, Kafulila arejeshwa kundini
Habari Mchanganyiko

Dk. Samia ateua viongozi 6, Kafulila arejeshwa kundini

Spread the love

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan leo Alhamisi ameteua viongozi mbalimbali akiwamo David Kafulila kuwa Kamishna wa Ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP). Kafulila alikuwa mkuu wa mkoa mstaafu wa Simiyu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kww mujibu wa taarifa iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano Ikulu Dodoma, viongozi wengine walioteuliwa ni Dk. Ellen Mkondya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Dk. Mkondya ni mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Benjamini Mkapa ya jijini Dar es Salaam.

Pia amemteua Justine Peter Mwandu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC). Mwandu ni mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Tanzania Reinsurance (TANRE).

Viongozi wengine walioteuliwa ni pamoja na Prof. Verdiana Grace Masanja kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI). Masanja ni Profesa wa Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela.

Amemteua Griffin Venance Mwakapeje kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania. Mwakapeje alikuwa Mkurugenzi Idara ya Huduma za kisheria kwa umma Wizara ya Katiba na Sheria.

Mwakapeje anachukua nafasi ta Casmir Kyuki ambaye atamaliza kipindi chake tarehe 7 Januari, 2023.

  Amemteua Fatma Mohamed Abdallah kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Puma Energy Tanzania. Abdallah ni mkurugenzi mtendaji wa Puma Energy – Geneva nchini Uswiss.

Abdallah anachukua nafasi ya Dominic Dhanah ambaye amemaliza muda wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!