Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Dk. Samia ataka mikakati kutokomeza unyanyapaa kwa WAVIU
AfyaHabari za Siasa

Dk. Samia ataka mikakati kutokomeza unyanyapaa kwa WAVIU

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan ameiagiza Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), wizara ya afya pamoja na wadau wengine kuweka mikakati ya kutokomeza ubaguzi na unyanyapaa kwa Watu wanaoishi na VVU (WAVIU). Anaripoti Mwandishi Wetu, Lindi … (endelea).

Pia katika suala la kuimarisha usawa, ameielekeza kuweka jitihada na mikakati madhubutu kuzuia maambukizi mapya na kuimarisha huduma za upimaji VVU na matumizi ya dawa za kufabaza VVU (ARVs) ili kutokomeza vifo vitokanavyo na Ukimwi.

Dk. Samia ametoa kauli hiyo loe tarehe 1 Disemba 2022 mkoani Lindi katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani.

Amesema maadhimisho hayo ambayo yanatimiza miaka 29 tangu janga la VVU, liingie nchini yanalenga kujitathmini, kukumbusha na kutafakari kwa pamoja, walipotoka, walipo na wanapoelekea katika mapambano dhidi ya VVU na hasa wakati huu ambapo Taifa na duniani kwa ujumla imedharimia kutokomeza VVU ifikapo mwaka 2030.

Akizungumzia kaulimbiu ya maadhimisho hayo ambayo ni ‘Imarisha Usawa’, ni mwendelezo wa kaulimbiu ya mwaka jana ambayo nayo ilikijita kwenye suala la usawa.

“Msisitizo wake mkubwa ni kuhimiza utoaji huduma za VV na Ukimwi ili kusiwe na maeneo au makundi ya watu yasiyofikiwa na huduma kisha kuondoa hali ya ubaguzi na unyanyapaa kwa watu wanaoishi na VVU.

“Hii inatokana na ukweli kwamba kukosekana kwa usawa kunarudisha nyuma juhudi zetu za kutokomeza ugonjwa huu ifikapo 2030,” amesema.

Amesema ni muhimu kutumia maadhimisho hayo kutafakari kwa kina na kuhakikisha wanaweka mikakati itakayoimarisha usawa ili lengo letu litimie.

“Lakini kuna jambo ambalo hatujalifanyia vizuri, suala zima la unyanyapaa bado haya mambo yapo ndio maana tumekuja na mikakati kuondosha unyanyapaa,” amesema.

Aidha, akizindua mkakati wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi wa mwaka 2022- 2026, ameagiza kila sekta iende kufanyia kazi ipasavyo.

Amesema mkakati huo ni safari ya kwenda kufikia malengo ya sifuri tatu.

Ameongeza kuwa kwa mwendo uliolezwa kwenye ripoti mbalimbali ni kwamba maambukizi mapya yanakua kwa vijana wenye umri kati miaka 15-24, hivyo ni vema kudhibiti maambukizi hayo ili kufikia lengo la kutokomeza VVU ifikapo 2030.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, George Simbachawene, amesema Tanzania imefanikiwa kupunguza maambukizi mapya ya Ukimwi kwa asilimia 50, pamoja na kudhibiti ambapo wanalioambukizwa wameanz akutumia dawa na kwamba wamebaki kama watu 200,000 kufikiwa na matibabu hayo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kupambana na Ugonjwa wa Ukimwi (UNAIDS), Winnie Byanyima, amesema Tanzania ni nchi iliyofanikiwa kupunguza maambukizi mapya ya ugonjwa huo kwa asilimia 50 miaka 12 iliyopita na kwamba asilimia 87 ya watu walioathirika wanapatiwa matibabu, kitendo ambacho kimeacha alama.

Amesema, mataifa ya Afrika yanapaswa kupunguza ombwe la jinsia katika maambukizi ya Ukimwi, kwa kuwa kati ya watu wanne walioambukizwa, watatu ni wanawake.
Amesema takwimu za 2021 zinaonyesha kati ya watu waliopata maambukizi katika mwaka huo, asilimia 30 walikuwa ni vijana wenye umri kuanzia miaka 14 hadi 25, ambapo vijana wa kike walikuwa asilimia 74 kati yao.

1 Comment

  • Watu wanaotunukiwa shahada ya udaktari za heshima huwa hawajiiti madaktari
    Mfano mmoja ni Barack Obama ambaye ametunukiwa Doctorate na vyuo 14 lakini hajiiti wala haitwi daktari
    Hata Mama Samia akisaifiri nje magharibi hataitwa daktari
    Tuache kujikwaza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!