Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari Dk. Samia asamehe wafungwa 1,631
HabariHabari Mchanganyiko

Dk. Samia asamehe wafungwa 1,631

Spread the love

KATIKA kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ametangaza msamaha kwa wafungwa 1,631 ikiwamo wa kike walioingia na mimba gerezani. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Aidha, amesema Rais Samia ametoa msamaha huo kwa kuzingatia mamlaka aliyopewa chini ya kifungu 45 (1) (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo wafungwa wenye sifa stahiki hupunguziwa robo ya adhabu zao baada ya punguzo la kawaida la moja ya tatu.

Kwa mujibu wa barua iliyotolewa jana tarehe 9 Desemba, 2022 na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni imeeleza kuwa chini ya kifungu cha 49 (1) cha sheria ya Magereza sura ya 58 wafungwa hao wawe wamehukumiwa kifungo cha miaka miwili au zaidi ambao wametumikia robo za adhabu zao magerezani.

Pia amesema wawe wameingia gerezani kabla ya Septemba 10, mwaka huu isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika sharti la 2, wafungwa wenye magonjwa ya kudumu au sugu ambao wapo hatua za mwisho za ugonjwa na hatua hiyo ithibitishwe na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa au Mganga mkuu wa Wilaya.

Amesema katika idadi tajwa wafungwa 101 wataachiliwa huru kuanzia Desemba 10, 2022 na 1530 watabaki gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha huo.

“Wafungwa wazee wenye umri wa miaka 70 au zaidi ambao wametumikia adhabu zao, umri huo uthibitishwe na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa na wa wilaya.

“Wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani au wenye watoto wanaonyonya na wasionyonya , wafungwa walemavu wa mwili na akili wasio na uwezo wa kufanya kazi na hali zao zidhibitishwe na jopo la uenyekiti wa Mganga Mkuu wa mkoa na wilaya.

“Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kuwekwa kizuizini ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka 15 au zaidi na wale waliohukumiwa kifungo cha maisha gerezani ambao wametumikia adhabu hiyo kwa miaka 20 au zaidi na waliobadilishiwa adhabu ya kifo na kuwa maisha na wamekaa miaka 20 au zaidi kuanza walipoanza kutumikia adhabu ya kifo,” amesema

Aidha, wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo kwa makosa ya kujamiana, utekaji au wizi wa watoto, kuwapa mimba wanafunzi au makosa yanayohusiana na ukatili dhidi ya watoto na biashara haramu ya binadamu ni miongoni mwa makundi ya wafungwa waliokosa msamaha huo.

“Waliokutwa na nyara za serikali, ujangili na kukutwa na viuongo vya binadamu, makosa ya ubadhilifu wa fedha za umma, wafungwa wa madeni (Civil Prisoners), unyang’anyi wa kutumia nguvu  na ule wa kutumia silaha, risasi, mlipuko au kujaribu kutenda makosa hayo.

“Msamaha huo haujawahusisha wafungwa waliohukimiwa adhabu ya kunyongwa na wenye makosa ya kujaribu kujiua au kuua watoto wachanga  na wanaotumikia vifungo vya nje chini ya sheria ya Bodi za Paroli sura ya 400(R.E.2002) sheria ya huduma kwa jamii sura 291(R.E. 2002) na kanuni za kifungo cha nje.

“Wengine waliokosa msamaha huo ni waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo kwa mashauriu/ kesi za uhujumu  uchumi na wanaotumikia  kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka ,utakatishaji wa fedha, rushwa, usafirishaji au kujiuhusisha  na  madawa ya kulevya ikiwemo bangi,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 12 wa kilo 726.2 za dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Spread the love  WATUHUMIWA watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari Mchanganyiko

GGML yasisitiza kuendelea kuimarisha afya za wafanyakazi

Spread the loveKAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited kwa kushirikiana na kampuni...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

error: Content is protected !!