May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Salim afikisha miaka 80, marais Samin Ramaphosa wamtakia kheri

Spread the love

 

MWANADIPLOMASIA mashuhuri nchini Tanzania, Dk. Salim Ahmed Salim leo Jumapili, tarehe 23 Januari 2022, ametimiza miaka 80 tangu alipozaliwa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Dk. Salima aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Tanzania na Katibu Mkkuu wa Umoja wa Nchi Huru Afrika (OAU) ambayo sasa ni Umoja wa Afrika (AU) alizaliwa tarehe 23 Januari 1942, visiwani Zanzibar.

Viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania, wamemtakia kheri mwanadiplomasia huyo ambaye kwa sasa anakabiliwa na tatizo la kiafya.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameweka picha ya Dk. Salima na kuandika, “Kheri ya siku ya kuzaliwa kwa Mheshimiwa Dkt. Salim Ahmed Salim, mtumishi mahiri wa umma wa Watanzania, Afrika na Dunia kwa zaidi ya miongo minne.”

“Katika siku hii adhimu ya kumbukumbu ya miaka 80 ya kuzaliwa kwako, tunakushukuru kwa utumishi uliotukuka kwa nchi yetu.

Naye Cyril Ramaphosa, Rais wa Afrika Kusini amempongeza na kumtakia kheri Dk. Salim akimwelezea kama mmoja wa kiongozi mashuhuri wa kuleta umoja barani Afrika, “na rafiki wa kweli kwa wananchi wa Afrika Kusini.”

error: Content is protected !!