May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Ndungulile: TCRA idhibiti ubora wa vifaa

Spread the love

 

DAKTARI Faustine Ndungulile, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuthibiti ubora wa vifaa vya kielektroniki kwa kuimarisha mfumo wa ukaguzi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Amesema, kwa kuimarisha mfumo huo, vifaa hivyo vitapata uhalali wa kutumika ndani ya mipaka ya Tanzania.

Ametoa kauli hiyo alipotembelea ofisi za mamlaka hiyo Zanzibar akiambatana na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Rahma Kassim Ali; Katibu Mkuu wake, Dk. Zainab Chaula na baadhi ya watendaji katika wizara hiyo.

Pamoja na kuweka mifumo hiyo, ameitaka TCRA kuweka alama kwenye vifaa hivyo itakayoonesha kuwa vimekaguliwa na kuthibitishwa.

Waziri huo ameeleza kutoridhishwa na TCRA namna inavyoelimisha wananchi na kwamba, mpaka sasa bado wananchi hawajaeleimika vya kutosha.

“Bado sijaridhishwa na kiwango cha elimu ya matumizi ya mtandao mnayoitoa kwa umma,” amesema Dk. Ndungulile na kuongeza “katika utoaji wa elimu kwa umma, mkumbuke kuelimisha jamii kuhusu wajibu na haki zao ili wanapopata shida mitandaoni, wajue wapite katika njia zipi.”

Alisema ikiwezekana vifaa hivyo viwekewe alama kuwa vimekaguliwa kuhakikisha usalama kwa matumizi ya wananchi.

error: Content is protected !!