October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Ndugulile azungumzia kutumbuliwa kwake

Dk. Faustine Ndugulile, aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya

Spread the love

DK. Faustine Ndugulile, amemshukuru Rais wa Tanzania, John Pombe Mangufuli kumteua kufanya kazi kama naibu waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)

Shukrani hizo za Dk. Ndugulile amezitoa leo Jumapili tarehe 17 Mei, 2020 kupitia akaunti yake ya Twitter ikiwa ni saa chache kupita tangu uteuzi wake ulipotenguliwa.

Jana Jumamosi, saa 2 usiku wa tarehe 16 Mei, 2020, Rais Magufuli alitangaza kumteua Dk. Godwin Mollel ambaye pia ni mbunge wa Siha (CCM) kuwa naibu waziri wa afya huku uteuzi wa Dk. Ndugulile ukitenguliwa.

Dk. Ndugulile ambaye ni mbunge wa Kigamboni kupitia CCM jijini Dar es Salaam, alihudumu katika nafasi ya naibu waziri kuanzia tarehe 9 Oktoba, 2017 akichukua nafasi ya Dk. Hamisi Kigwangalla aliyeteuliwa kuwa waziri wa maliasili na utalii.

“Nimepokea uamuzi wa Mhe Rais kwa unyenyekevu mkubwa. Ninamshukuru sana JPM kwa kunipa fursa ya kuhudumu katika Serikali yake.”

“Nawashukuru sana @umwalimu na watendaji wote kwa ushirikiano walionipatia. Mafanikio ya sekta ni makubwa sana. Namtakia kila la kheri NW ajaye Dkt Mollel.,” ameandika Dk. Ndugulile.

Malcolm @shilinde_cc amechangia ujumbe huo wa Dk. Ndugulile akisema,”Utumishi wako uliotukuka umeonekana, Watanzania wameona, you can be proud of that.,”

Naye fredy @fredy08122355 amesema,”Endelea kuwatumikia wapiga Kura wako, kazi uliyopewa, uliifanya kwa weledi mkubwa, hongera Sana Dr! ulikuwa miongoni mwa viongozi wanyenyekevu sana.”

error: Content is protected !!