Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Maisha Afya Dk. Ndugulile atembelea MOI, akagua chumba cha tiba mtandao
Afya

Dk. Ndugulile atembelea MOI, akagua chumba cha tiba mtandao

Dk. Faustine Ndungulile, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (katikati) akikagua wodi ya kutibu kwa mtandao
Spread the love

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile ametembelea Taasisi ya Tiba ya mifupa, upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu (MOI) kukagua maendeleo ya chumba maalum cha Tiba mtandao ambacho kinatarajia kukamilika na kufanya kazi kuanzia mwezi Juni mwaka huu. Anaripoti Hamisi Mguta … (endelea).

Awali akiwa kwenye taasisi hiyo ya MOI, Dk. Ndugulile aliweza kupokea maendeleo ya ukamilishwaji wa chumba hicho cha tiba mtandao ambapo pia aliwataka kuhakikisha wanasimamia vizuri uendeshaji wake kwani utasaidia Taifa kutoa huduma za kibingwa sehemu kubwa zaidi hapa nchini zikiwemo hospitali za rufaa za mikoa na nyingine 

Aidha, Dk. Ndugulile amewataka kukamilisha hatua zote za chumba hicho na kitakapokamilika uzinduzi ufanyike kama inavyotarajiwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dk. Respicious Boniface amesema kuwa, chumba hicho kinategemea kukamilika na kuanza kufanya kazi mwezi Juni mwaka huu na kitakapokamilika kitasaidia matibabu kwa kwa njia ya mtandao nchi nzima.

“Chumba cha Tiba mtandao hapa MOI kitakapokamilika hospitali zote kubwa za rufaa za mikoa na zingine za Rufaa, zitatuma picha hapa na watalaam wa MOI wanatoa majibu na kurudisha tiba kule na kutoa ushauri wa jinsi wa kutoa matibabu kwa wagonjwa wakiwa hukohuko,” alieleza Dk. Boniface.

Chumba hicho cha tiba mtandao kinatarajiwa kuwepo kwenye jengo jipya la MOI ambapo tayari timu ya watalaam wanaendelea na taratibu za kukamilisha uendeshaji wake.

MOI ni miongoni mwa Taasisi za tiba zenye kutoa huduma za kibingwa huku ikiwa na Madaktari wabobezi kwenye tiba ya mifupa, upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Waziri wa Tamisemi apewa siku 14 afike Morogoro kutatua changamoto za Afya

Spread the love  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel...

Afya

Ma-RMO, DMO watakiwa kujitafakari ubadhirifu hospitali za mikoa, wilaya

Spread the love  NAIBU Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel, amewataka waganga...

Afya

JK atoa ya moyoni kuhusu huduma za afya

Spread the love  RAIS Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete amesema huduma za afya...

AfyaHabari za Siasa

Heche amvaa Ummy Mwalimu kisa bima ya afya

Spread the love  MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chadema, John Heche amemtaka...

error: Content is protected !!