May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Ndugulile aitaka TCRA isikwamishe usajili vyombo vya habari

Dk. Faustin Ndungulile

Spread the love

 

WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile, ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), isikwamishe utoaji leseni za usajili kwa wawekezaji wanaotaka kufungua vituo vya redio, maeneo ya vijijini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Ndugulile ametoa agizo hilo leo Jumamosi, tarehe 31 Julai 2021, katika uzinduzi wa mfumo wa kielektroniki wa utoaji leseni wa TCRA, uliofanyika mkoani Dar es Salaam.

Waziri huyo wa mawasiliano amesema kuwa, Serikali imepanga kutoa leseni za redio katika wilaya 69 za vijijini na pembezoni mwa nchi, ili kuimarisha usikivu katika maeneo hayo.

“Tunataka kuwekeza hususan usikivu wa redio, tulitangaza jana wilaya 69 Watanzania wajitokeze kuomba leseni katika wilaya hizo ambazo hazina usikivu. Hatutaki kuona wanakwazwa kwa sababu ya leseni, tunaka leseni zitolewe kwa muda mfupi bila kuwakwaza,” amesema Dk. Ndugulile.

Naye Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa, ameagiza mamlaka hiyo kukamilisha maboresho ya mfumo wa ukusanyaji mirabaha ya wasanii, uliyopo katika kanzi data ya Chama cha Hakimiliki (COSOTA).

“Kuna jukumu la la COSOTA katika data center (kituo cha data), kuhakikisha mfumo wa kukusanya mirabaha ya wasanii inaboreshwa ,” amesema Bashungwa.

error: Content is protected !!