June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Dk. Nagu anatuangusha Urais’

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Dk. Mery Nagu

Spread the love

WANANCHI wilayani Hanang katika Mkoa wa Manyara wanasema, wamesikitishwa na kitendo cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Dk. Mery Nagu kutojitokeza kuchukua fomu ya kuwania urais kama alivyokusudia. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Wakizungumza na MwanaHALISI online kwa wakati tofauti wamesema kuwa, ilikuwa ni makusudio ya wananchi wa wilaya hiyo kumuona mbunge wao akijitosa katika kiny’ang’anyoro hicho.

Mmoja wa wanachi aliyezungumza na gazeti hili ni Sikay Bura ambaye amesema, wananchi wa Mkoa wa Manyara hususani Hanang walitegemea kuona Dk. Nagu akichukua fomu ya kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera kwa ajili ya kuwa rais kupitia CCM.

Lanta Momoy amesema, ni faraja kubwa kwa wananwake ambao wanaonesha ujasiri wa kuongoza nchi huku akisema walimwamini Dk. Nagu kutokana na uzoefu wake katika uongozi.

“Dk. Nagu amekuwa kiongozi ndani ya serikali zaidi ya mika 20 hivyo tuliamini zaidi kama angechukua fomu angeweza kupata nafasi kubwa kulingana na uzoefu wake.

“Tuliamini kuwa, ataweza kuchukua fomu na sisi tulimuoamba muda mrefu akwa ametukubalia lakini cha kushangaza hadi sasa haajachukua fomu na muda ndo huo katibu unaisha sasa sijui itakuwaje,” amesema.

Kwa upande wake Qamdiya Bughay amesema, iwapo Dk. Nagu hatochukua fomu kwa ajili ya kuomba ridhaa ya kuwa rais ni wazi kuwa, wananchi watakuwa wamepata masikitiko makubwa.

“Kimsingi tulitegemea sana kuona Dk. Nagu akichukua fomu ili awe mwanamke wa tatu kati ya wale ambao wamechukua fomu kwa ajili ya kupeperusha bendera ya kuusaka urais kupitia CCM.

“Hata hivyo kwa siku hizi zilizobaki tunaendelea kumsii na kumuomba ili aweze kuchukua fomu jambo ambalo tunaamini kuwa litaweza kuwa ni faraja kwetu ambao tunamtegemea leo” amesema.

Kwa upande wake Dk. Nagu alipotafutwa ili kueleza kama atachukua fomu au la! amesema “anasubiri matakwa ya wananchi ambao wanaona kuwa nafaa kupeperusha bendera ya kuwa rais.”

Mpaka sasa wagombea 36 tayari wamechukua fomu kati ya hao wanawake ni wanne na iwapo Dk. Nagu atachukua fomu, atatimiza idadi ya wanawake watano.

error: Content is protected !!