Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mwinyi: Sitofukua makaburi, lakini…
Habari za Siasa

Dk. Mwinyi: Sitofukua makaburi, lakini…

Dk. Hussein Mwinyi, Mgomnbea Urais Zanzibar (CCM)
Spread the love

RAIS wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK), Dk. Hussein Mwinyi amesema, hatojali mtoto wa mtu katika maamuzi magumu atakayochukua ingawa hatofukua makaburi. Anaandika Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Akizungumza katika Ukumbi wa Fiedel Castro, Chakechake visiwani humo leo tarehe 17 Desemba 2020, wakati wa kutoa shukrani zake kwa wanachama na taasisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema Wazanzibari wasitaharuki kwa maamuzi atakayochukua.

“Katika kuhakikisha ahadi zetu tulizotoa zinakamilika, nataka niseme katika kipindi hiki cha kwanza lazima tutafanya maamuzi magumu. Naomba mtulie, msitaharuki, nataka kukuhakikishieni maamuzi nitakayofanya yana lengo moja tu, kuthibiti.

“Sitafuti mchawi wala sifukui makaburi lakini yako mambo tusipoyafanya kwa maamuzi magumu, huko tunakokwenda nako ni kugumu,” amesema Dk. Mwinyi huku akiwataka wakazi wa visiwa hivyo viwili (Unguja na Pemba) kumvumilia.

Amesema, serikali yake haina uvumilivu na watu wala rushwa, wahujumu uchumi pia wanaokula mali ya umma kwa kuwa, asipofanya sasa, mbele ya safari itakuwa tabu.

Rais huyo amesema, Zanzibar kila mtu unayeweza kumgusa, unaweza kuambiwa ‘ni mtoto wa fulani’ na kwamba hilo kwake hatolizingatia.

Na kwamba, muda aliokaa madarakani tayari kila eneo alilogusa, linanuka rushwa na kwamba, nchi inaendelea kufilisiwa kwa vitendo vya ufisadi.

Mwenyekiti huyo wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar amesema, ili kutimiza ahadi zake alizotoa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, lazima achukue uamuzi mgumu hasa baada ya kushuhudia uozo.

Dk. Mwinyi amesema, lengo la uamuzi huo ni kuhakikisha anadhibiti matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maendeleo.

“Leo tunazungumzia miradi ya maendeleo ya fedha nyingi, tunazungumzia miradi ya maendeleo ya fedha nyingi, zaidi ya Dola za Marekani Mil. 93 zinakwenda katika mradi wa maji unaonedelea.

“Na kuna miradi itakayokuja inayogharimu Dola 110 Mil. tusipochukua maamuzi magumu sasa, hizi fedha zitafujwa,” amesema na kuongeza:

“Iko miradi  ya maji, umeme na barabara. Nataka niahidini tutaisimami ili tuweze kupata thamani katika fedha tutakazotoa.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!