May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Mwinyi, Maalim Seif ni ‘kazi kazi’ Z’bar

Spread the love

KAZI ya kumwaga sumu ya ubaguzi miongoni mwa Wazanzibari, inayofanywa na Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na makamu wake wa kwanza Maalim Seif Sharif Hamad, sasa inashika kasi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pemba…(endelea).

Wakati Dk. Mwinyi akiwaambia wakazi wa Pemba kwamba, lengo la Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), visiwani humo ni kuimarisha amani, Maalim Seif amewaambia wakazi hao kuwa suala la amani sio la hiyari.

Dk. Mwinyi na Maalim Seif wametoa kauli hiyo wakati walipozungumza kwenye mkutano wa mkuu wa pili wa amani uliofanyika Unguja tarehe 16 Januari 2021.

Dk. Mwinyi ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar amesema, anachokitaka kwenye serikali yake ni kudumisha na kuimarisha amani, umoja na mshikamano kwa Wazanzibari wote.

Dk. Mwinyi amewaambia wajumbe wa mkuano huo kwamba, Katiba ya Zanzibar yam waka 1984, imetoa kipaumbele kikubwa katika suala la amani.

Na kwamba, atafanya awezalo kuhakikisha malengo ya waasisi wa taifa hilo kuhusu amani, umoja na mshikamano yanafikiwa kwa manufaa ya ustawi wa viziwa hivyo viwili.

Wakati huo, Maalim Seif ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, amesema maridhiano hayo yanapaswa kulelea na kuwa na tija ili vizazi vijavyo viweze kusoma historia na kurithi.

Chama cha ACT-Wazalendo mwishoni mwa mwaka jana, kiliridhia kujumuika katika kuunda SUK, licha kushutumu chama tawala -Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kuvuruga uchaguzi uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2021.

Awali, ACT-Wazalendo kiligoma kushiriki kwenye serikali hiyo licha ya kupata zaidi ya silimia 10 ya kura iliyohitajika na Katiba ya Zanzibar ili kuingia kwenye muundo wa seikali.

Mabalozi wa Nchi za Ulaya waliohudhuria mkutano huo, wameeleza kuwa na matumaini makubwa ya Zanzibar kupiga hatua kutokana na hatua za awali kuchukuliwa.

error: Content is protected !!