Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mwinyi kuingia Ikulu leo
Habari za Siasa

Dk. Mwinyi kuingia Ikulu leo

Spread the love

DAKTARI Hussein Ali Mwinyi, leo Jumatatu tarehe 2 Novemba 2020 ataapishwa kuwa Rais wa nane wa Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea)

Shughuli hiyo ya uapisho, itafanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo Dk. Mwinyi mwenye miaka 53 anachukua nafasi inayoachwa wazi na Rais Ali Mohamed Shein.

Rais Shein, anamaliza ungwe yake ya miaka kumi ya utawala kwa mujibu wa Katiba aliyoianza tarehe 3 Novemba 2010.

Dk. Mwinyi ambaye ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, anaapishwa baada ya kutangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuibuka mshindi wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 27 na 28 Oktoba 2020.

          Soma zaidi:-

Dk. Mwinyi alitangazwa tarehe 29 Oktoba 2020 na Mwenyekiti wa ZEC, Jaji Hamid Mahmoud Hamid kwa kupata kura 380,402 sawa na asilimia 76.27 ya kura zote 382,402.

Jaji Hamid alisema, Maalim Seif Sharif Hamad wa ACT-Wazalendo alipata kura  99,103 sawa na asilimia 19.87.

Dk. Mwinyi atakuwa Rais wa nane wa visiwa hivyo tangu kufanyika kwa Mapinduzi ya Zanzibar tarehe 12 Januari 1964.

Dk. Mwinyi aliyezaliwa tarehe 23 Desemba 1966 ni mtoto wa Ali Hassan Mwinyi, aliyekuwa Rais wa Zanzibar kwa siku 267 kisha Rais wa Tanzania kati ya mwaka 1985 hadi 1995.

Marais wengine walimtangulia na miaka yao kwenye mabano wa kwanza ni;  Abeid Karume (26 Aprili 1964- 7 Aprili 1972), Aboud Jumbe (7 Aprili 1972- 30 Januari 1984), Ali Hassan Mwinyi (30 Januari 1984- 24 Oktoba 1984), Idris Abdul Wakil (24 Oktoba 1985- 25 Oktoba 1990).

Salmin Amour (25 Oktoba 1990- 8 Novemba 2000), Aman Abeid Karume (8 Novemba 2000- 3 Novemba 2010) na Dk. Ali Mamohed Shein aliingia 3 Novemba 2010 hadi leo Jumatatu anapokabidhi madaraka kwa Dk. Mwinyi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yaiangukia Serikali kunusuru wananchi Liwale, Nachingwea

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari za Siasa

Gridi ya Taifa kufumuliwa kukabiliana na katizo la mgao wa umeme

Spread the love  WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba, amesema Serikali ina mpango...

error: Content is protected !!