September 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Mwinyi azitaka halmashauri kuchukua madawati

Spread the love

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,  Dk. Hussein Mwinyi amezitaka halmashauri ambazo hazijachukua madawati, kufanya haraka kuchukua, anaandika Pendo Omary.

Amesema, vinginevyo wizara hiyo itazishauri mamlaka za juu zigawe upya madawati hayo kwa maeneo mengine yenye uhitaji.

Tarehe 11 Aprili mwaka huu, jeshi hilo lilipewa zabuni na serikali kutengeneza madawati 60,000 kwa gharama ya Sh. 3 Bilioni ambapo  bei ya kila dawati ni Sh. 50,000.

Dk. Mwinyi ametaja maeneo ambayo hayajachukua madawati hayo kuwa ni Kikindi, Pangani, Makambako, Ludewa, Wangingome na Makete, Iringa Mjini,  Mbeya Mjini, Mbeya Vijijini, Ileje, Kyela, Rungwe na Busokelo, Tunduru Kaskazini.

Maeneo mengine ni Sogwe mkoani Sogwe pia Kwela, Nkasi Kaskazini na Nkasi Kusini.

“Jumla ya madawati ambayo hayajachukuliwa mpaka sasa ni 9, 666.  Hatua ya kutochukua madawati hayo inafanya: madawati yaliyo tayari yanaendelea kupigwa jua na kuna uwezekano wa kunyeshewa mvua.

“Yameziba nafasi ya kuhifadhi madawati mengine tunayotengenezwa hivyo kukinzana na dhana ya kutatua tatizo la madawati,” amesema Dk. Mwinyi.

Amesema, mpaka sasa madawati ambayo yamechukuliwa ni 22, 721, kati ya madawati 30, 000 ya awamu ya kwanza.

 

error: Content is protected !!