July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Mwinyi amteuwa kiongozi Yanga

Spread the love

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ally Mwinyi amemteuwa Arafat Ally Haji ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji na Mwenyekiti wa kamati ya fedha na mipango ya klabu ya Yanga, kuwa Mkurugezni Mwendeshaji wa Shirika la Bima la Zanzibar. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Arafati ameteuliwa na Dk. Mwinyi, ikiwa katika kipindi cha karibia na mwaka mmoja, tangu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dk. Mshindo Msolla kumteuwa kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo ya fedha ikiwa na wajumbe saba.

Kamati hiyo iliteuliwa tarehe 1 julai 2019, huku Makamu Mwenyekiti akiwa Shijja Richard na Katibu Deo Mutta.

Wajumbe wa Kamati hiyo ni Said Kambi, Ally Mayay, Pindu Luhoyo, Baraka Katemba, Suma Mwaitenda, Haruna Batenga na Ivan Tarimo.

Licha ya kuwa Mwenyekiti wa kamati ya fedha ndani ya Yanga, laini pia Arafa ni mfanyakazi wa Benki ya Exim.

Dk. Mwinyi pia amefanya uteuzi wa Hemed Seleiman Abdulla kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uratibu na udhibiti wa Dawa za Kulevya, na pia amemteuwa Asaa Ahamada Rashid kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

 

error: Content is protected !!