Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Mwinyi aishukuru AfDB kwa kuunga mkono maendeleo Zanzibar
Habari Mchanganyiko

Dk. Mwinyi aishukuru AfDB kwa kuunga mkono maendeleo Zanzibar

Dk. HUssein Mwinyi, Rais wa Zanzibar
Spread the love

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ally Mwinyi , ameishukuru Benki ya Maendeleleo ya Africa (AfDB) kwa kuunga mkono miradi mbalimbali ya maendeleo ya Zanzibar ikiwemo ya kijamii, afya, barabara, maji na sekta ya usafirishaji. Anaripoti Judith Laurent (DSJ) … (endelea).

Rais Mwinyi ametoa shukrani hizo leo tarehe 27 Februari 2023 ambapo ameeleza maendeleo juu ya hatua zinazoendelea kupigwa na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar katika kusimamia sekta zilizo chini ya uchumi wa buluu.

Kwa upande wa utalii Rais Mwinyi amesema unachangia hadi asilimia 30 za pato la nchi huku akikiri kuwa kwa upande wa uvuvi bado kuna changamoto ya matumizi ya mbinu za kizamani za uvuvi.

Kuhusu kilimo hususani cha Mwani amesema inaonesha kuwa kilimo hicho kinaendeshwa zaidi na wanawake , ambao wanahitaji kusaidiwa ili kuendeleza ubora zaidi utakao walaetea pato kubwa kulinganisha na sasa.

Kwa upande wake Rais wa AfDB, Dk. Akimwumi Adsena, amemweleza Dk. Mwinyi kuwa miradi ambayo benki hiyo inasaidia zaidi ni ujenzi wa miundombinu ikiwemo barabara ili kurahisisha sekta ya usafirishaji.

“Kwa sasa benki inasaidia maendeleo ya ujenzi unaoendelea wa barabara ya Hububu, Mahonda,Mkototoni, Barabara ya Tunguu , Makunduchi hadi Chakechake” amesema Dk. Adsina.

Pia amesema benki hiyo imejitoa kusaidia maendeleo hayo na kuunga mkonon juhudi zote za harakati za kimaendeleo kwa kutenga milioni 15 kwa kuunga mkono sekta hizo katika kuendelea kukuza uchumi wa buluu nchini

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!