July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Mwinjaka kutumbua jipu TRL

Spread the love

KUKOSEKANA kwa nyongeza ya mishaha, makato yao kutopelekwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na kukosekana kwa mkataba wa hali bora, kumechochea mgogoro kati ya wafanyakazi wa Kampuni Reli ya Tanzania (TRL) na uongozi wa kampuni hiyo. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Tayari mgogoro huo umefikishwa mezani kwa Katibu Mkuu wa Wizira ya Uchukuzi, Dk. Shaabani Mwinjaka ambapo unatarajiwa kupatiwa ufumbuzi Alhamisi wiki hii.

Wakizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa TRL (TRAWU) wamesema kuwa, oungozi huo ulifikisha malalamiko, kero na madai ya muda mrefu kwa mkuregenzi wa TRL, Elias Mshana na kupuuzwa.

Katibu Mkuu wa TRAWU, Boazi Nyakeke ameeleza kuwa, waliandamana na uongozi wa chama hicho mpaka kwa Dk. Mwinjaka ambapo ahadi ya utatuzi wa mgogoro huo imetajwa kukamilika Alhamis wiki hii.

Mwenyekiti wa (TRAWU), Mussa Kalala amesema kuwa wafanyakazi wa kampuni hiyo wamechoshwa na mzigo wa kero zinazowaelemea ambapo wana madai yanayofanana nchi nzima kutokana na ufisadi mkubwa unaofanywa na uongozi wa shirika hilo.

error: Content is protected !!