October 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Mwakyembe: Msijifiche kwangu kumsema Lowassa

Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Michezo

Spread the love

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe, amewataka wanasiasa kuacha kujificha mgongoni kwake kwa lengo la kumshambulia Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, Edward Lowassa. Anaandika Mwandishi Wetu … (endelea).

Dk. Mwakyembe ametoa onyo hilo leo wakati akihojiwa na kituo cha redio cha Clouds FM kuhusu taarifa iliyosambazwe kwenye mitandao ya kijamii ikionesha imetoka kwake kwamba atapambana na Lowassa katika sakata la Richmond.

“Taarifa ile haikuwa ya kwangu,  ni upuuzi. Mnanijua kwamba huwa sikurupuki. Mimi ni waziri wa Serikali ambaye naheshimu wadhifa wangu, hivyo siwezi kuandika mambo kama hayo. Nilipigiwa simu hata na wenzangu wakiniuliza mbona nimeandika maneno makali,”amesema.

Kwa mujibu wa Dk. Mwakyembe, hana sababu ya kuendelea kujadili swala la kashfa ya Richmond kuhusu Lowassa.

“Kama ni suala la kashfa ya Richmond, jamani mbona tulimtanguliza Mungu? Tulifanya kazi yetu kwa haki na ripoti ya Bunge ipo. Sasa hakuna haja ya unafiki…unafiki wa watu kutaka kumsema Lowassa halafu wanajificha mgongoni kwangu,” amesema.  

Amesema amekwisha kamilisha hatua za awali za kutoa taaria katika mamlaka zinazohusika ikiwemo Polisi Makao Makuu Kitengo cha uharifu wa kimtandao (Cyber Crime), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili waweze kubaini mtandao huo ambao ulianza harakati zake tangu Lowassa atangaze nia.

“Sio uungwana kuchezea majina ya watu wanaokosa ujasiri wa kuelezea hisia zao hadi watumie majina ya watu wengine, mtandao huo nauona kuwa ni hatari,” amesema na kuongeza kuwa huenda kwa sababu ya joto la uchaguzi ndio maana suala hilo likapewa msukumo.

Dk. Mwakyembe ametamba kuwa, “nimedhamiria kukomesha tabia hii, nimekwenda Polisi Kitengo cha Cyber Crime (Mkosa ya Jinai ya Mtandao) na TCRA, kulalamikia mchezo huu hatari wa kihuni na tayari vyombo hivi vimeanzisha uchunguzi huu mkali, ili kubaini wahusika wote wanaoandaa hizo taarifa na kuzituma kwenye sehemu mbalimbli na wanaozituma sehemu nyingine hizo taarifa, lakini lazima tupeleke ujumbe ulio wazi kwa sababu nchi yetu inaendeshwa kwa misingi ya sheria”.

error: Content is protected !!