Friday , 1 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Mwakyembe: Marufuku magazeti kuswoma kwenye redio na tv
Habari MchanganyikoTangulizi

Dk. Mwakyembe: Marufuku magazeti kuswoma kwenye redio na tv

Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Spread the love

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harison Mwakyembe amepiga marufuku watangazaji wa vipindi vya magazeti kwenye redio na televisheni kusoma habari zote bali wasome vichwa vya habari pekee sababu kufanya hivyo kumeonekana kuanza kuua soko la magazeti, anaandika Christina Haule.

Akizungumza jijini Mwanza katika kilele cha maadhimisho ya 26 ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari duniani Dk. Mwakyembe ametaka agizo hilo lianze kutekelezwa mara moja bila kupigwa ili kutoua soko la magazeti na kupoteza maana halisi ya vyombo vya habari.

Aidha amesema suala la kusoma habari kama ilivyoandikwa kwenye magazeti si nzuri kwani inaua soko la magazeti.
Hata hivyo amesema kuwa atahakikisha katika uongozi wake waandishi makanjanja hawana nafasi ili kazi ya uandishi wa habari izidi kuwa na heshima.

Aidha amesema, atahakikisha anawalinda waandishi wa habari hasa wanaoandika habari za uchunguzi na wanaofanya kazi kwa weledi hivyo inapotokea changamoto ni vyema waandishi kujilinda huku wakijizuia kutobebwa na wanasiasa.

Dk. Mwakyembe amesema kalamu ya mwandishi inatetea na kuharibu maisha ya mtu na taifa hivyo itumike kwa weledi.

“Tuna kazi ya kuhakikisha tasnia ya habari inaheshimika, kwa sasa makanjanja hawatakuwa na nafasi labda Yesu arudi,’’ amesema Dk. Mwakyembe.

Amesema ulinzi wa mwandishi unaanzia kwa Mungu kwa kuwa wanakazi ngumu katika jamii na wanaweza kujenga au kubomoa hivyo kuna kila sababu kwa waandishi wa habari hapa nchini kuhakikisha hawapindishi ukweli kwa ajili ya maslahi binafsi.

“Tusibebe hisia na kuacha taaluma, kama kuna jambo ni vizuri waandishi wakafanya uchunguzi na kubaini usahihi wa jambo, hiyo inasaidia kuchukua hatua,’’ amesema.

Aidha Dk. Mwakyembe anesema kuwafungia viongozi kwa kutoandika habari zao si njia sahihi kwa kuwa kunawanyima wananchi haki ya kupata habari kutoka kwao.

Amesema yuko tayari kama kuna kiongozi mwenzie wa serikali ambaye amekosema katika chombo cha habari kukaa pamoja na yeye kushiriki katika mazungumzo hayo ili kumaliza changamoto iliyopo.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Kusini mwa Afrika (MISATAN), Salome Kitomari amesema matukio ya utekwaji nyara na viwango vya unyanyaswaji wa wanahabari duniani yameonekana kuongezeka hasa kwa wafanyakazi wa kawaida kwenye vyombo vya habari.

Amesema mwaka jana hapa nchini kumeripotiwa kesi za manyanyaso na ukiukwaji wa uhuru wa vyombo vya habari zaidi ya 30 zinazohusisha magazeti kufungiwa, kusimamishwa kwa leseni waandishi kupigwa na kuwekwa rumande kwa mashauri tofauti ambayo hayana msingi wa kisheria.

“Tukio la kukamatwa kwa mwandishi wa ITV na Radio One mkoani Arusha, Halfani Liundi, kuwapo kwa vitisho vingi vya kuuawa kwa waandishi kuzuiwa kupata
taarifa kwenye baadhi ya ofisi za Umma,’’ amesema Kitomari.

Amesema miongoni mwa matukio hayo ni kushambuliwa na kujeruhiwa kwa takribani wanahabari saba waliokwenda kuripoti habari za kundi mojawapo kati
ya mawili yanayovutana ndani ya Chama cha CUF.

Katika maadhimisho hayo wanahabari wameadhimia kuwa habari ni biashara ngumu isiyo na faida hivyo hatua ya serikali kuweka utaratibu wa matangazo yake kudhibitiwa kupitia MAELEZO itaathiri tasnia hivyo wakae pamoja na wadau .

Aidha makubaliano hayo ni pamoja usalama wa wanahabari kusimamiwa ipasavyo, vyombo vya habari vya kijamii, vyenye hali mbaya zaidi kufutiwa usajili wa kibiashara na utawala wa sheria uendeleze uhuru wa mawazo na kuleta maendeleo endelevu.

Siku ya Uhuru wa Vyombo Vya Habari Duniani inaadhimishwa kila Mei 03 ili kutathmini kanuni za msingi za uhuru wa habari na kujieleza na kufanya tathmini na mwaka huu kauli mbiu ni Fikra makini katika nyakati changamoto Jukumu la vyombo vya habari kudumisha amani usawa na jamii jumuishi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mwili wa Hayati Mwinyi kuagwa leo saa 8 Uwanja wa Uhuru

Spread the loveMWILI wa Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi unatarajiwa kuagwa kuanza...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

Spread the loveMWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania,...

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

error: Content is protected !!