November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Msolla amrudisha Madega Yanga

Dk. Mshindo Msolla, Mwenyekiti wa Yanga

Spread the love

MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Dk. Mshindo Msolla ameteua wanachama nane wa klabu hiyo akiwemo Wakili Iman Madega kuunda Kamati ya Mabadiliko ya Katiba kuelekea kwenye mfumo wa mabadiliko ya uwendeshaji wa klabu hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Yanga ambayo tarehe 2 Desemba, 2020, ilipokea rasimu ya mabadiliko ya uwendeshaji wa klabu hiyo kutoka kwa kamati ya mabadiliko iliyokuwa chini ya Wakili Alex Mgongolwa aliyeongozana na meneja wa mradi huo Mhandisi Hersi Said.

Mara baada ya kupokea rasimu hiyo mwenyekiti wa klabu hiyo, Dk. Msolla alisema kuwa wataunda kamati maalumu ya kufanya mabadiliko ya katiba ili iweze kuruhusu kwenda katika mfumo wa uwendeshaji timu wa kisasa tofauti na awali na baadae kuipeleka kwa wanachama kupitia mkutano mkuu.

Taarifa ya leo tarehe 8 Desemba, 2020 kutoka ndani ya klabu ya Yanga ilionesha majina ya wanachama walioteuliwa kuunda kamati hiyo ambayo itaongozwa na Wakili Raymond Wawa.

Wengine ni Wakili Madega, Wakili Sam Mapande, Wakili Audats Kahendagile, Wakili Mark Anthony, Mohammed Msumi, Pastory Kiyombia na Debora Mkemwa.

Yanga ambayo kwa sasa ipo kwenye mchakato wa mabadiliko ya uwendeshaji kwa kuipeleka timu hiyo kwenye mfumo wa kampuni ambapo wanachama watakuwa wanamiliki hisa asilimia 51, huku wawekezaji wakimiliki hisa asilimia 51.

Kwa kufanya hivi Yanga itakuwa timu ya pili kwenye ukanda wa Afrika Mashariki kufanya mabadiliko ya uwendeshaji mara baada ya Simba kuwa katika hatua za mwisho kukamilisha mchakato huo ambapo muwekezaji wake Mohammed Dewji ataweka kiasi cha pesa Sh. 20 bilioni.

error: Content is protected !!