September 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Mponda awapa ahueni wananchi

Spread the love

KITUO cha Afya cha Mtimbila wilayani Malinyi, Morogoro kimekabidhiwa mashine ya kufulia na kukausha nguo yenye thamani ya Sh. 4.7 Milioni ili kuwasaidia wananchi hasa wanawake kuondokana na adha ya kufua nguo za wagonjwa wao wenyewe, anaandika Christina Haule.

Mashine hiyo imetolewa na Dk. Haji Mponda, Mbunge wa Jimbo la Malinyi wakati wa siku ya usafi ambayo hufanyika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi nchi nzima.

Akipokea mashine hiyo Dk. David Maziku, Mganga Mkuu wa kituo hicho cha Afya amemshukuru Mbunge huyo kwa kuona umuhimu wa kuwapatia mashine hiyo inayoweza kuwasaidia kufua na kukausha mashuka baada ya kutumiwa na wagonjwa.

“Mashine hii itatusaidia sisi kama kituo cha afya pamoja na wananchi ili kuepukana na adha ya kufua mashuka ya hospitali ambapo ndugu wa wagonjwa walilazimika kufua kutokana na uchache wa wahudumu,” amesema Dk. Maziku.

Dk. Mponda, Mbunge wa jimbo hilo amesema kuwa aliguswa na adha wanayoipata wagonjwa katika jimbo lake na ameamua kutoa mashine hiyo ikiwa ni sehemu ya majukumu yake kama mtumishi aliyechaguliwa na wananchi wote.

“Nasukumwa na dhamira ya dhati ya kuleta mabadiliko ya kweli kiuchumi na kijamii katika jimbo hili na naahidi kuwa, licha ya wingi wa changamoto katika sekta ya afya lakini nitashughulikia kwa awamu hadi kuzimaliza kabisa changamoto hizi,” amesema.

Mashine iliyotolewa na mbunge huyo ina uwezo wa kufua mashuka 100 kwa siku kufuatia kufua 14 kilogramu  za nguo ambazo ni sawa na wastani wa mashuka 20 hadi 30 kwa mara moja ambapo kazi hiyo mashine hufanya kazi hiyo ndani ya saa 2.

 

error: Content is protected !!