Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mpango: Siri ndiyo uhai wa Serikali
Habari za Siasa

Dk. Mpango: Siri ndiyo uhai wa Serikali

Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango
Spread the love

 

MAKAMU wa Rais nchini Tanzania, Dk. Philip Mpango, amewataka Wakuu wa Wilaya kote nchini kudhibiti uvujaji wa siri za serikali kwa kuepuka kutuma nyaraka za Serikali kwenye mitandao ya kijamii. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea)

Dk. Mpango amesisitiza kuwa Wakuu hao wa Wilaya wanapaswa kuzingatia kuwa “siri ndiyo uhai wa Serikali.”

Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu tarehe 13 Machi 202, wakati akifungua mafunzo ya siku sita kwa Wakuu wa Wilaya yanayoendelea jijini Dodoma.

“Jambo la pili mtakuwa na mada kuhusu utunzanji wa siri za Serikali, jambo hili ni kuhimu sana hasa katika kipindi cha utandawazi na matumizi ya mitandao ya kijamii kwahiyo itawapasa mzingatie kuwa siri ndiyo uhai wa serikali hivyo ni lazima kudhibiti uvujaji wa siri za Serikali, epukeni kabisa kuitumia mitandao ya kijamii kama vile Whatsapp na email binafsi kutuma nyaraka za Serikali,” amesema Dk. Mpango.

Aidha Dk. Mpango amesisitiza kuhusu matumizi ya walinzi na waandishi wa habari binafsi na kusema kuwa upo utaratibu wakufuata endapo itabainika kiongozi anahitaji watumishi hao.

Amesema viongozi kujipatia watumishi hao bila kufuata taratibu za Serikali kuna hataraisha usalama wao na hata wa siri za Serikali.

“Kumekuwepo watu wanajichukulia walinzi binafsi na waandishi wa habari binafsi katika ofisi za umma, sasa zipo taratibu za kufuta endapo itabainika kiongozi anahitaji kupatiwa wasaidizi wa aina hii kwahiyo zinagatieni taratibu zilizopo na si vinginevyo,” amesisitiza.

Vilevile amewataka Wakuu wa Wilaya ambao pia ni Wenyeviti wa Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya, kuwa makini na maneno wanayozungumza na wasaidizi wao hususani madereva na watu wengine wanapokuwa nje ya ofisi hata sehemu za starehe ili kuepuka kutoa siri za Serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!