May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Mpango kuapishwa kesho Ikulu-Dodoma

Dk. Philip Mpango, Makamu wa Rais Tanzania

Spread the love

 

DAKTARI Philip Isdor Mpango, kesho Jumatano tarehe 31 Machi 2021, saa 9:00 alasiri, ataapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Dk. Mpango, aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango, anaapishwa baada ya kupendelezwa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kuwa makamu wa Rais.

Rais Samia amewasilisha jina la Dk. Mpango leo Jumanne tarehe 30 Machi 2021, bungeni kupitia kwa mapambe wale na Bunge limemthibitisha kwa kura zote za wabunge 363 waliohudhuria sawa na asilimia 100.

Mara baada ya Bunge kumthitibisha, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa amesema, hafla ya kuapishwa kwa Dkt. Mpango mwenye miaka 63 itafanyika Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma.

Msigwa amesema, Dk. Mpango ataapishwa kushika wadhifa huo baada ya Rais Samia, kuwasilisha mapendekezo ya jina lake kuwa Makamu wa Rais katika Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi.

error: Content is protected !!