Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mpango: Bashe acha ubahili toa hela za utafiti
Habari za Siasa

Dk. Mpango: Bashe acha ubahili toa hela za utafiti

Spread the love

MAKAMU wa Rais, Dk. Philip Mpango amemuagiza Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kuacha ubahili na kuhakikisha wizara hiyo inatoa fedha za kutosha kufanya utafiti katika masuala ya kilimo kwani bila utafiti kilimo kitakufa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Pia amemuagiza waziri huyo kuandaa mkakati maalumu wa kutengeneza vifungashio, kwa sababu kila anapoenda anakumbana na kilio cha vifungashio hafifu.

Amesema mkakati huo unatakiwa kuhusisha wizara ya viwanda na biashara, Shirika la Viwango nchini (TBS) pamoja na wadau wa kilimo biashara ili kupata vifungashio bora vinavyoendana na soko la mazao ya kilimo duniani.

Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango leo tarehe 1 Agosti, 2022 wakati akifungua maonesho ya sherehe za sikukuu ya wakulima ‘nanenane’ ambayo kitaifa yanafanyika Uyole mkoani Mbeya katika viwanja vya John Mwakangale.

Akitembelea mabanda katika maonesho hayo, Dk. Mpango alimhoji mmoja wa wawakilishi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kituo cha Naliendele kama wamepatiwa fedha za utafiti ambapo alijibu kwamba mwaka jana walipatiwa lakini mwaka huu hawajapatiwa fedha hizo.

Kutokana na majibu hayo, Dk. Mpango alimugiza Bashe kuhakikisha fedha za utafiti zinatolewa haraka ili kuimarisha shughuli za utafiti wa kilimo nchini.

“Lazima tuthamini utafiti, utatusaidia kuongeza thamani katika kilimo, mathalani mabibo tulikuwa tunayatupa lakini Naliendele sasa wanayatafiti, bila kutafiti tutaendelea kulima kienyeji,  waziri waambie na wenzako ule ubahili ndani ya wizara waache,” amesema.

Ametolea mfano kuwa utafiti umesaidia kubaini kuwa kuna maziwa ya korosho jambo ambalo Watanzania wengi walikuwa hawajui, hivyo sasa hata mtoto asiye na meno anaweza kupewa korosho kupitia maziwa ya zao hilo.

Kwa mujibu wa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2022/2023, imeongezeka kutoka Sh bilioni 294,1 hadi Sh bilioni 751.1, bajeti ya masuala ya utafiti imetengwa Sh bilioni 40.7.

1 Comment

  • Duh!
    Bashe anaua kilimo ili iweje?
    Hii ni hatari kwa uhuru wa nchi yetu na inaweza kuwa sababu ya kuwapa watu wa nje mashamba yetu.
    Hakuna nchi inayowapa watu wa nje kilimo chao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!