October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Mpango azitaka mamlaka maliasili utalii kukomesha urasimu vibali

Spread the love

MAKAMU wa Rais Dk. Philip Mpango ameziagiza mamlaka zinazoshuhulikia masuala maliasili na utalii kuondoa urasimu katika utoa wa vibali katika sekta hiyo. Anaripoti Juliana Assenga (UDSM)…endelea

Dk. Mpango ametoa maagizo hayo leo Jumanne tarehe 17 Agosti, 2022, katika hafla ya ugawaji magari 44 ya mradi wa uendelezaji maliasili na utalii Kusini (REGROW) iliyofanyika katika hifadhi ya Mikumi mkoani Morogoro.

Amesema yapo malalamiko yanayotolewa na wadau wa utalii kwa mamlaka zinazosimamia sekta ya utalii katika utoaji wa vibali na huduma mbalimbali.

“Baadhi ya wadau wamekuwa wakitoa malalamiko kuhusu dorasi hizo…hili la urasimu katika utoaji wa vibali iwe mwisho,” amesisitiza Dk. Mpango na kuzitaka mamlaka zenye dhamana kuchangamkia fursa zaidi na kutatua changamoto zilizopo.

Mbali na hayo amesisitiza umuhimu wa kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwani nchi zilizoendelea zimefanikiwa kutangaza vivutio vya utali ndani na nje ya nchi zao, “tuwe wabunifu kama alivyofanya Rais wetu na tusiishie tu kwenye mlima Kilimanjaro na Serengeti.”

Aidha aliitaka TANAPA kuziangalia kwa jicho la kipekee hifadhi za Taifa za Mikumi na Saadani ili ziweze kupata watalii wengi kutokana na kuwa karibu na Dar es Salaam ambalo amesema ni lango la wageni kuingia nchini.

Sambamba na hilo ametoa wito kwa sekta binafsi kuwekeza katika miundombinu ya utalii ikiwemo kujenga hoteli nzuri kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watalii wanaotembelea Tanzania.

Makamu Rais pia amesema upo umuhimu wa kutunza na kutangaza fursa na rasilimali zilizopo katika mikoa yetu ambayo bado haijatangazwa ambapo amewataka wakuu wa mikoa na wilaya zote, kuhamasisha katika suala la utalii wa ndani.

Aidha Dk. Mpango amekemea juu ya suala la uharibifu wa mazingira hususani katika maeneo ya hifadhi unaosababishwa na utupaji taka, ufugaji wa kuhama hama na utupaji wa vishungi vya sigara vinavyosababisha moto.

Mpango amezitaka wizara ya ardhi, maliasili na utalii pamoja na TAMISEMI kushirikiana na wadau wengnie kuacha upimaji wa maeneo yaliyo karibu na hifadhi kwani yamekuwa yakisababisha malumbano na hata kupelekea baadhi ya wananchi kufariki.

error: Content is protected !!