Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Dk. Mpango awaomba viongozi wa dini kuliombea Taifa
Habari Mchanganyiko

Dk. Mpango awaomba viongozi wa dini kuliombea Taifa

Spread the love

 

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango amewaomba viongozi wa dini na waumini kwa ujumla kuendelea kuliombea Taifa pamoja na viongozi wake ili waongozwe na hekima ya Mungu katika kuwatumikia wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Njombe … (endelea).

Dk. Philip Mpango ameyasema hayo leo tarehe 3 Aprili, 2022 aliposhiriki Ibada ya Misa Takatifu ya domonika ya tano ya Kwaresma katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yoseph, Jimbo Kuu Katoliki la Njombe, ibada ilioongozwa na Mhashamu Askofu John Ndimbo.

Aidha, Makamu wa Rais amewapongeza wananchi wa Mkoa wa Njombe kwa utunzaji na usafi wa mazingira na kuwahimiza kuendelea kulinda na kutunza mazingira mazuri yanaowazunguka.

Kwa upande wake Mhashamu Askofu John Ndimbo amemshukuru Makamu wa Rais kwa kushiriki ibada hiyo na kumuhakikishia kwamba kanisa Katoliki kwa miaka mitatu limetoa kipaumbele cha pekee katika uhifadhi wa mazingira kwa kuzingatia umuhimu wake kwa maendeleo endelevu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mawakili waiburuza mahakamani TLS, EALS

Spread the love  WAKILI Hekima Mwasipu na wenzake wawili, wamefungua kesi katika...

Habari Mchanganyiko

Uvuvi bahari kuu wapaisha pato la Taifa

Spread the love  SERIKALI imesema uvuvi wa bahari kuu umeliingizia Taifa pato...

Habari Mchanganyiko

DPP aweka pingamizi kesi ya ‘watu wasiojulikana’

Spread the love  MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), ameweka pingamizi dhidi ya...

Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the loveKAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa...

error: Content is protected !!