Sunday , 5 February 2023
Home Kitengo Maisha Afya Dk. Mpango ataka wezi wa dawa wataifishwe
Afya

Dk. Mpango ataka wezi wa dawa wataifishwe

Spread the love

 

MAKAMU wa Rais wa Tanzania, Dk. Phillip Mpango, ameiagiza Wizara ya Afya itaifishe mali za wezi wa dawa na vifaa tiba vya Serikali, ili kufidia hasara wanayosababisha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mtwara … (endelea).

Dk. Mpango ametoa agizo hilo leo Jumatatu, tarehe 26 Julai 2021, akiweka jiwe la msingi katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini, mkoani Mtwara.

“Kwa maana hiyo mtumishi yeyote ambaye tutambaini amehusika na wizi wa dawa na vifaa vyake, cha kwanza muondoeni kazini, msiishie hapo vyombo vya sheria vipo mpelekeni mahakamani. Tutaifishe chochote alichonacho kufidia upotevu wa dawa zetu,” amesema Dk. Mpango.

Kuhusu ujenzi wa hospitali hiyo, Dk. Mpango ameliagiza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kumaliza kwa wakati ujenzi wake ili ianze kazi kwa muda uliopangwa.

“Nitumie nafasi hii kuwataka NHC ujenzi huu ukamilike kwa wakati, kama ilivyopangwa mwezi Oktoba huduma ianze,” amesema Dk. Mpango.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dk. Maulidi Banyani, amesema ujenzi wa hospitali hiyo unagharimu Sh. 15.8 bilioni, ambapo hadi sasa Serikali imeshatoa Sh. 14.1 bilioni.

Dk. Banyani amesema kuwa, ujenzi wa hospitali hiyo ulioanza Septemba 2019, umefikia asilimia 97, na kuwa hadi kufikia tarehe 29 Septemba mwaka huu, itakabidhiwa serikalini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Waziri wa Tamisemi apewa siku 14 afike Morogoro kutatua changamoto za Afya

Spread the love  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel...

Afya

Ma-RMO, DMO watakiwa kujitafakari ubadhirifu hospitali za mikoa, wilaya

Spread the love  NAIBU Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel, amewataka waganga...

Afya

JK atoa ya moyoni kuhusu huduma za afya

Spread the love  RAIS Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete amesema huduma za afya...

AfyaHabari za Siasa

Heche amvaa Ummy Mwalimu kisa bima ya afya

Spread the love  MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chadema, John Heche amemtaka...

error: Content is protected !!