May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Mpango ataja sifa za kiongozi bora

Dk. Philip Mpango, Makamu wa Rais wa Tanzania

Spread the love

 

MAKAMU wa Rais wa Tanzania, Dk. Philip Mpango amesema, kiongozi yoyote ili aweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo lazima awe hodari wa kazi na awe mfano kwa tabia. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).

Dk. Mpango, ametoa sifa hizo leo Jumatano, tarehe 19 Mei 2021, mara baada ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kumaliza kuwaapisha wakuu wa mikoa na taasisi mbalimbali waliokuwa amewateua hivi karibuni.

“Kiongozi ni lazima awe na sifa mbili, awe hodari wa kazi na awe mfano kwa tabia. Hatuwatarajii viongozi mliopewa dhamana na mliopo, ni muhimu sana tukienda huko kwenye vituo vya kazi, tusiwe na tabia nzuri. Sitarajii kuwa na walevi au wazinzi,” amesema Dk. Mpango

Pia, amesema, mbali na jukumu la wakuu wa mikoa kuwa wenyeviti wa kamati ya ulinzi na usalama, “lakini ni kusimamia uchumi wa mikoa yenu kwa umakini zaidi. Ni muhimu kujielekeza kuongeza uchumi na tija kwa kuangalia masoko ya wananchi.”

“Msitumie madaraka yenu vibaya, msionee watu, mkatende haki. Kila mmoja kwenye eneo lake, kuheshimu sheria na kuzifuata,” amesema

Naye Spika wa Bunge la Tanzania, amewaonya wakuu wa mikoa na wilaya, amboa wamekuwa na tabia ya kujiita wao ni marais wa maeneo hayo kutokufanya hivyo.

“Wapo wakuu wa mikoa na wilaya, wakiwa huko wanasema mimi ni Rais wa mkoa huu, mimi Rais wa wilaya hii, Rais wa nchi hii ni Mama Samia Suluhu Hassan, ukijivisha mimi ni rais, unajivisha koti ambalo si lako,” amesema Spika Ndugai

error: Content is protected !!