June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Mpango amng’oa mkurugenzi Nanyumbu kwa tuhuma za ubadhirifu

Dk. Philip Mpango, Makamu wa Rais wa Tanzania

Spread the love

 

MAKAMU wa Rais wa Tanzania, Dk. Phillip Mpango, amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara, Hamis Dambaya, kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha zinazomkabili. Anaripoti Mwandishi wetu, Mtwara … (endelea).

Dk. Mpango alichukua hatua hiyo jana tarehe 24 Julai 2021, baada ya kutembelea ujenzi wa stendi ya mabasi ya Mangaka iliyopo wilayani huo na kubaini ubadhirifu wa fedha.

Makamu huyo wa rais, alibaini ubadhirifu huo baada ya kuona ujenzi wa stendi hiyo unaogharimu Sh. 2.2 bilioni,  haulingani na thamani ya fedha husika.

“Unajua vitu vingine ukiona huwezi kazi,  awamu hii ya sita jiondee mwenyewe. Lakini nitafuatilia mpaka hii hela ipatikane, Serikali imetoa  Sh.  2.2  bilioni hapa halafu unasema huongo? Mvua ikinyesha maji yanatuama,  mimi siridhiki na matumizi ya hizi hela,” alisema Dk. Mpango.

Dk. Mpango amemuagiza Naibu waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Dk. Festo Dugange, kusimamia suala hilo, ili fedha zilizofujwa zirudishwe.

“Ofisi ya Rais-Tamisemi naagiza zirejeshwe,  zirudi hizo pesa za hawa masikini, kinachoonekana wamechezewa katika hili jengo. Hebu angalieni miaka mitano hela inaliwa hapa na wewe unaangalia kila siku,” alisema Dk. Mpango.

error: Content is protected !!