MAKAMU wa Rais, Dk. Phillip Mpango, ameutaka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), kupitia upya sheria za utoaji vibali vya kuvuna mazao ya misitu, ili kudhibiti ukataji holela wa miti kwa ajili ya shughuli za kibinadamu hususan mkaa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Dk. Mpango alitoa agizo hilo tarehe 12 Januari 2023, katika kilele cha upandaji miti kilichoendana na kumbukumbu ya miaka 59 ya mapinduzi ya Zanzibar, jijini Dodoma.
“Ikibidi mpitie upya sheria za utoaji wa vibali vya kuvuna mazao ya misitu ambavyo vitawezesha utunzaji wa mazingira kwa lengo la kuboresha mazingira kwa kuongeza wingi wa kupanda miti,” alisema Dk.Mpango.
Katika hatua nyingine, Dk. Mpango aliagiza Halmashauri ya Jiji la Dodoma, kuwapa adhabu kali ikiwemo faini, watu watakaokutwa na makosa ya kufanya uharibifu wa mazingira.
Wakati huo huo, Dk. Mpango aliziagiza halmashauri zote nchini kupanda miti isiyopungua milioni 1.5, kwa ajili ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira kwa wananchi.
Safi Sana. Naomba Halmashauri zipande miti ya asili na siyo ya kigeni.
Wangeweka utaratibu ambao hauumizi mwanaichi na siyo sheria ipitiwa upya na uamuzi hapo hapo bira kuwasikiriza wanachi mimi ni najishugurisha na kusafirisha mkaa reseni ya kusafirishia ninayo na kibari nakatia ira tumesimamishwa gafura na tunamikopo na mikataba ya pikipiki tunavunia kibaha na kureta dar wengeweka utaratibu na siyo gafra ivo
Naombeni vyombo vya habari wariingirie kati sheria ipitiwe na kazi ienderee uamuzi ukipatikana taratibu zitafatwa na kazi ziendere tupewe muda nipo bunju