May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Mpango aapishwa makamu wa Rais Tanzania

Dk. Philip Mpango, Makamu wa Rais wa Tanzania akiapa mbele ya Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma

Spread the love

 

JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, amemwapisha Dk. Philip Isdor Mpango, kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Dk. Mpango (63), ameapishwa leo Jumatano, tarehe 31 Machi 2021, Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.

Hafla hiyo imehudhuliwa na viongozi mbalimbali akiwemo, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Dk. Mpango ameapishwa baada ya jana Jumanne, jina lake kuwasilishwa Bungeni jijini Dodoma na kuithibitishwa kwa kura za wabunge wote 363 waliohudhulia kikao hicho sawa na asilimia 100.

Dk. Mpango ameapishwa kuchukua nafasi ya Rais Samia, ambaye yeye aliapishwa kuwa Rais wa Tanzania kuchukua nafasi iliyokuwa imeachwa na Dk. John Pombe Magufuli.

Dk. Philip Mpango, Makamu wa Rais wa Tanzania akiapa

Dk. Magufuli, alifariki dunia tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya mfumo wa umeme wa moyo.

Mwili wa Dk. Magufuli ulizikwa nyumbani kwao, Chato mkoani Geita.

error: Content is protected !!