Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Mpango aagiza Ma-RC, DC kuwaondoa waliojenga kwenye vyanzo vya maji
Habari Mchanganyiko

Dk. Mpango aagiza Ma-RC, DC kuwaondoa waliojenga kwenye vyanzo vya maji

Spread the love

MAKAMU wa Rais Dk. Philip Mpango amewaagiza wakuu wilaya na mikoa kushirikiana na mamlaka zingine kuwaaondoa wananchi wote wanaoishi na kuendesha shughuli za uchumi kama vile kilimo na mifugo maeneo ya milima iliyopo karibu na vyanzo vya maji. Anaripoti Kenneth Ngelesi, Mbeya … (endelea).

Dk. Mpango ametoa agizo hilo mkoani Mbeya leo tarehe 16 Novemba, 2022 wakati wa akizindua kampeni ya kupanda miti rafiki na vyanzo vya maji lililofanyika katika chanzo cha maji cha Nzovwe jijini Mbeya ambapo miti milioni mbili inatarajiwa kupandwa.

Aidha, ameiagiza wakala wa huduma za misitu nchini TFS kuhakikisha wanatambua miti rafiki na maji kulingana na eneo husika ikiwa ni pamoja na kuandaa vitalu na miche ya kutosha na kuipanda katika vyanzo vya maji kwenye mikoa yote badala ya kuwa na miti ya kibiashara pekee.

Wakati huo huo Dk. Mpango amefungua mkutano mkuu wa nane wa mwaka wa bodi za maji za mabonde uliofanyika mkoani Mbeya na kuwaagiza wadau wa mazingira wa kiwemo NEMC kuacha kutoa vibali vya kufanya shughuli za kiuchumi kwenye maeneo ya vyanzo vya maji.

Wakati Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson amesema ni vema TFS kupanda miti ya asili badala ya miti ya kibiashara ambayo ikifiki wakati wa kuvuna eneo linakiuwa wazi.

Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Waziri wa Maji Juma Aweso, Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Dk. Sulemani Jaffo, wakuu wa mikoa kutoka mikoa ya Nyanda za Juu kusini pamoja na wakuu wa taasisi za kisekta na Wakurugenzi watendaji wa mabonde yote tisa nchini

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!