Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Michezo Dk. Mkwizu: Afrika tudumishe utamaduni
Michezo

Dk. Mkwizu: Afrika tudumishe utamaduni

Spread the love

 

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Mkoa wa Kilimanjaro (ALAAT), Dk. Salehe Mkwizu ameshauri nchi za Afrika kudumisha utamaduni wa bara hilo kwa kuwa ndio urithi usiofutika na endelevu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morocco … (endelea).

Mkwizu amesema hayo wakati akihutubia mkutano wa Mameya wa Afrika unaoendelea jijini Rabat nchini Morroco.

Mkutano huo umehudhuriwa  na mameya 54, mabalozi na mawaziri kutoka nchi zote za Afrika ambapo Tanzania imewakilishwa na Mkwizu ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga.

Dk. Mkwizu alisema hadi sasa Afrika imeshindwa kufanya mambo mengi ya pamoja kama kuanzisha benki yao, fedha moja na mengineyo.

“Tumekuwa na visingizio vingi katika kuanzisha fedha ya pamoja na mengine, je sasa na hili la kushindwa kulinda tamaduni zetu tutamsingizia nani? Ni wajibu wetu kulinda, kudumisha na kuukuza utamaduni wa Kiafrika kwa maisha bora ya vizazi vyetu vijavyo.

Agenda ya utamaduni ni agenda namba nne ya maendeleo katika Taifa lolote hivyo kama Afrika kuanzia agenda ya kwanza mpaka ya tatu zinatusumbua je na hii ya nne ambayo inatuhusu kwa asilimia 100 bila kutegemea mataifa ya magaharibi nayo tutasema kwa nini imetushinda kuheshimu, kulinda na kudumisha utamaduni wetu? Au katika hili tutarudi tuseme watuwezeshe fedha?’’ alihoji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

Michezo

Ujanja ni kubeti na Meridianbet

Spread the love  JUMAPILI ya leo imekaa kihela hela sana ndani ya...

error: Content is protected !!