Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mashinji: Nichagueni mimi, Kawe Tuna jambo letu
Habari za Siasa

Dk. Mashinji: Nichagueni mimi, Kawe Tuna jambo letu

Dk. Vincent Mashinji
Spread the love

ALIYEKUWA katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendelea (Chadema), Dk. Vincent Mashinji amewaomba wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kawe kumchagua awe mgombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa tatehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Mashindi amesema hayo leo Jumanne tarehe 21 Julai 2020 wakati akijinadi kwa wajumbe wa mkutano huo wa maoni wenye lengo la kumpata mgombea ubunge wa jimbo hilo linaloongozwa na Halima Mdee wa Chadema.

Mdee amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa kipindi cha miaka kumi mfululizo kuanzia mwaka 2010 hadi sasa.

Bosi huyo wa zamani wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini humo ni miongoni mwa wagombea 170 wanaowania nafasi hiyo akiwemo Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Kamapuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Francis Nanai.

Dk. Mashinji ni mtia nia namba 161 kati ya watia nia 170 waliofika kila mmoja kujinadi wakitumia dakika moja kumwaga sera.

“Kawe tuna jambo letu na jambo hilo ni kuhakikisha tunarejesha jimbo la Kawe, nina nguvu na hali zaidi ya kurejesha jimbo hili kuliko wenzangu wote” amesema Dk. Mashinji

Naye bosi wa zamani wa MCL, Nanai amesema amekuwa mkazi wa 20 na miaka saba ameitumikia kampuni hiyo lakini ameamua kuiacha ili kutatua matatizo ya wana Kawe.

“Nimeacha kazi hii kwa sababu ya machungu niliyoyaona na shida katika jimbo letu. Naomba tuungane kumchagua Francis Majige Nanani,” amesema

Wajumbe wote wamemaliza kujinadi na sasa shughuli inayoendelea ni upigaji kura.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kwa habari zaidi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!