Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mashinji awa kikwazo kesi ya Mbowe, wenzake 
Habari za Siasa

Dk. Mashinji awa kikwazo kesi ya Mbowe, wenzake 

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imeahirisha kesi ya uchochezi inayowakibili viongozi waandamizi wa Chadema, kutokana na mshtakiwa namba sita kutokuwepo. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Mshatakiwa wa sita kwenye kesi hiyo ni Dk. Vicent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chama hicho. Wengine ni Freeman Mbowe, Mwenyekiti Chadema- Taifa; John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu – Bara; Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar; John Heche, Mbunge Tarime Vijijini.

Pia yumo Ester Matiko, Mbunge wa Tarime vijijini; Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini na Halima Mdee, Mbunge wa Kawe.

Leo tarehe 16 Aprili mwaka 2019, Prof. Abdallah Safari ameongoza jopo la mawakili wa utetezi, aliwasilisha barua ya udhuru ya Dk. Mashinji mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya kusikilizwa.

Profesa Safari akisaidiwa na Wakili Peter Kibatala, Hekima Mwasibu, Jeremia Mtobesya na John Mallya amewasilisha barua hiyo aliyoilekezwa kwa Hakimu Simba ambapo mshatakiwa ameomba ruhusa ya mahakama kutokana na kuwepo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Songea.

Na kwamba, yupo Songea kuhudhuria kesi ya uchochezi inayomkabili kwenye mahakamani hiyo.

Prof. Safari akinukuu barua hiyo, ameeleza kuwa kesi hiyo namba 9 ya mwaka 2017, imefika katika hatua ya utetezi na kwamba, ameridhia kuendelea kwa usikilizwaji wa kesi inayomkabili katika Mahakama ya Kisutu.

Wakati huo huo, Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi amedai kuwa, kutokuwepo kwa mshtakiwa wa sita kumeibua hoja ya kuombwa mahakama kuendelea na usikilizwaji wa kesi.

“Ni Rai ya upande wa mashtaka kuwa, taarifa ya mshitakiwa haina vidhibitisho vya kutufanya sisi tukubaliane nayo.

“Ninasema hivyo kwa sababu, tangu tarehe ya mwisho ya kutajwa kesi hiyo inafika wiki mbili sasa na  siku ya mwisho mshtakiwa alikuwepo mahakamani. Tulitegemea mshtakiwa angeijuza mahakama kuwa, ana kesi mahakama ya Songea,” ameleeza Nchimbi na kuongeza;

“Atuambie, kigezo gani alitumia asije kwenye mahakama hii na kwenda Songea ikiwa alikuwepo hapa angeweza kuiambia mahakama. Aje ajieleze na aieleze mahakama hii.”

Amedai, tarehe ya mwisho shauri hilo lilipotajwa, lilikuja kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji na kwamba, upande wa mashtaka uliandaa mashahidi kwa ajili ya usikilizwaji.

Wakili Nchimbi ameeleza mahakamani hapo kuwa, utaratibu wa kisheria umeelekeza kwenye sheria ya  mwenendo wa makosa ya jinai (CPA), shauri lolote la jinai ikifika sehemu ya kuchukua ushahidi, ni lazima ushahidi unapochukuliwa mahakami, uchukuliwe mbele ya mshtakiwa au washtaka.

Amedai, licha ya fungu la 197 (1b) sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai linatoa mwanya kwa kutoa ushahidi, isipokuwa mshitakiwa anapokuwa ana matatizo ya kiafya, na awe anawakili pia awe ameridhia.

Hakimu Simba ameahilisha shauri hilo mpaka kesho tarehe 17 saa 4 kamili asubuhi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!