September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Makongoro Mahanga afariki dunia

Spread the love

DAKTARI Milton Makongoro Mahanga, aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam, amefariki dunia alfajiri ya leo tarehe 23 Machi 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa za kifo hicho zimetolewa mapema leo  na Jerome Olomi, Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilaya ya Ilala.

Olomi amesema Chadema inaendelea kuwasiliana na ndugu wa marehemu kwa ajili ya kujua taratibu za mazishi, kisha kitatoa taarifa baadae kuhusu msiba huo.

“Habari makamanda, taarifa mbaya tusizozitegemea tulizozipata asubuhi hii mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Ilala Dr Milton Makongoro Mahanga  amefariki dunia. Tutazidi kupeana taarifa za taratibu nyingine,” inaeleza taarifa ya Olomi.

Dk. Makongoro kabla umauti kumfika alikuwa Mwenyekiti wa Chadema wilayani Ilala, awali alikuwa mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

error: Content is protected !!