October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Makakala: Chuo cha uhamiaji chachu maendeleo, usalama

Spread the love

 

KAMSHINA Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dk. Anna Makalala amesema kuanzishwa kwa Chuo cha Uhamiaji kutakua ni chachu ya maendelo na usalama dhidi ya bishara haramu ya usafirishaji wa binadamu nchini. Anaripoti Apaikunda Mosha, TUDARCo … (endelea).

Ameyasema hayo leo Jumatatu tarehe 15 Agosti, 2022 wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi katika chuo cha uhamiaji na kufunga mafunzo ya askari wa uhamiaji kozi namba 1 ya mwaka 2021-2022.

Hata hivyo ameishukuru serikali kwa kuongeza bajeti ya mwaka ya chuo kiasi cha Sh 600 milioni kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za wakufunzi na kuongeza bajeti ya maendeleo kutoka kiasi cha Sh 45.5 bilioni hadi kufikia Sh 93.6 bilioni kwa mwaka 2022-2023.

Amebainisha kuwa serikali imesaidia kulipa deni kiasi cha Sh 8.9 bilioni kwa ajili ya watumishi na wazabuni, pia serikali imewezesha chuo kiasi cha Sh 900 milioni kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala, ulinzi, zahanati na mabweni saba.

Ameongeza kwa kusema mafanikio mengine ambayo jeshi la uhamiahaji limepata kwa muda mchache ambao Rais Samia amekuwa madarakani ni pamoja na Rais kuridhia idara ya uhamiaji kupata hadhi ya kuwa jeshi kwa mujibu wa sheria ikiwa pamoja na kupata stahiki za kijeshi na kutunikiwa nishani kwa askari na maafisa wa uhamiaji, kibali cha ajira kwa idadi kubwa ya askari 818 na kupandishwa vyeo maafisa, askari na watumishi ndani ya chuo.

Aidha ameiomba serikali kuongeza miundombinu mbalimbali ili kuimarisha uwezo ikiwemo ukubwa wa rasilimali watu vyombo vya usafiri, nyumba za makazi ya maafisa na askari wa uhamiaji, ofisi za wilaya, vituo mipakani na huduma ya maji safi na salama ndani ya chuo.

Aidha, Dk. Makakala amemshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye amesaidia kupatikana kwa huduma ya umeme wa TANESCO ndani ya chuo na maji safi kutoka kwenye vyanzo vya maji mjini Tanga.

error: Content is protected !!