July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Makaidi kuzikwa kesho

Spread the love

MWILI wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha National League for Democracy (NLD) ambaye pia alikuwa mgombea ubunge Jimbo la Masasi mkoani Mtwara, Dk. Emmanuel Makaidi aliyefariki Alhamis, wiki iliyopita, unatarajiwa kuzikwa kesho Makaburi ya Sinza jijini Dar es Salaam. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Dk. Makaidi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), alifariki wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Nyangao baada ya presha yake kupanda ghafla ikiwa nyumbani kwake mjini Masasi wakati akijiandaa kutekeleza ratiba yake ya shughuli za kampeni ya uchaguzi.

Katibu wa Ukawa, Dk. George Kahangwa ameliambia gazeti la MwanaHALISI Online kwamba, “mazishi ya kitaifa ya Dk. Makaidi yatafanyika katika ukumbi wa Karimjee kuanzia saa 5 asubuhi, maziko yatakuwa katika makaburi ya Sinza kuanzia saa 8:30 mchana.”

“Mazishi haya yatahudhuriwa na mgombea urais kupitia Ukawa, Edward Lowassa, viongozi wa kitaifa wa serikali, Ukawa, vyama vya siasa na michezo,” amesema Kahangwa.

error: Content is protected !!