August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Mahanga: Magufuli anaua demokrasia aliyoikuta

Dk. Makongoro Mahanga, aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Kazi

Spread the love

DAKTARI Makongoro Mahanga, aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Kazi ameshangazwa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli akisema, ni utawala uliojipambanua kwa kuminya na kukandamiza demokrasia hapa nchini, anaandika Pendo Omary.

Mahanga ameuambia mtandao wa MwanaHALISI Online kuwa, vyama vya upinzani kuzuiliwa kufanya siasa, wanachama wa upinzani kunyanyaswa ndani ya nchi yao mithili ya wakimbizi ikiwemo kuwekwa mahabusu kinyume na sheria, ni vitendo ambavyo havikuwepo katika awamu ya nne.

“Awamu ya nne wapinzani waliheshimiwa kwa kiasi kikubwa. Walisikilizwa na hata baadhi ya maoni yao yalikubaliwa na serikali lakini kwa sasa hivi serikali hii inawaona wapinzani wa kisiasa kama maadui wa nchi au waasi,” anasema Dk. Mahanga.

Mahanga ambaye kwa sasa ni mwenyekiti Chadema katika Mkoa wa kichama wa Ilalà, jijini Dar es Salaam, amesema wakati wa serikali ya awamu ya nne wabunge, viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani walingia ofisi za mawaziri bila vikwazo na kutoa mawazo na maombi yao kwa serikali lakini kwa sasa ni marufuku.

“Kwa sasa wanakataa. Wanaogopa hata kuongea na viongozi wa upinzani kwenye simu au kuwakaribisha ofisini kwao. Mimi ni shuhuda wa hili. Ninajiuliza; Iweje leo CCM na serikali yake iwaone wapinzani kama maadui wakubwa kuliko hata Al-Shabaab?” amehoji Dk. Mahanga.

error: Content is protected !!