Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Magufuli: Wana Muleba msirudie makosa
Habari za Siasa

Dk. Magufuli: Wana Muleba msirudie makosa

Spread the love

DAKTARI John Magufuli, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amewataka wananchi wa Kata ya Kasharunga wilayani Muleba, Bukoba kutorudia kosa la kuchagua wagombea wa upinzani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Muleba … (endelea).

Dk. Magufuli ambaye ni Rais wa Tanzania anayemaliza muda wake, ametoa kauli hiyo leo tarehe 15 Septemba 2020 wakati anawanadi wagombea wa CCM wilayani humo.

“Nafahamu tulikuja tukawoamba kura na mimi nilipita hapa nikamuomeba kura mgombea ubunge bahati nzuri mlipa wa CCM, nikaomba mumpe diwani wa CCM bahati mbaya mambo hayakwenda hivyo mkasema hapana.

Lakini kwa sababu nchi hii ya demokrasia na sisi ni wavumilivu tukasema mtoto akikosea haumkati mkono mtu akifanya makosa husamehewa,” amesema Rais Magufuli.

Mgombea huyo wa CCM katika nafasi ya Urais amesema kutokana na msamaha huo, aliamua kutoa kiasi cha Sh. 500 Mil. kwa ajili ya kujenga Hospitali.

“Nilipoletewa bajeti kwenye kata hii inataka hospitali nilitoa Mil. 500 nikajenga hospitali, nasikia aliyekuwa diwani hapa alisema alileta yeye,” amesema Dk. Bashiru.

Aidha, Rais Magufuli amesema aliamua kujenga hospitali hiyo kwa sababu aliona wananchi wanateseka ilhali walimchagua kuwa rais na Mbunge wa Muleba Kusini, Anna Tibaijuka, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

“Tuliamua tujenge hii hospitali sababu wananchi tuliona wanateseka lakini walimchagua Tibaijuka na mimi huwezi kumhukumu kwa kosa dogo watoto wateseke, pamoja na maji tatizo tulianza kuleta hospitali, lakini katika miaka mitano ijayo tutaleta maji,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amewaomba wananchi wa Kasharunga kuwachagua wagombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

“Kosea njia, kosea kuoa au kuolewa unaweza kutoa talaka au kukataa mume lakini usikosee kuchagua, saa nyingine mnanipa shida kusaidia jimbo unakuta diwani ukisema CCM oye anakunyooshea vidole viwili, amesema Rais Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!