December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Magufuli: Sikustahili urais

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS John Magufuli amesema kuwa, hakustahili kuwa Rais wa Tanzania bali Watanzania wenyewe ndio waliomchagua. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Amesema, wananchi wa Mbarali mkoani Mbeya na maeneo mengine ya nchi, ndio walimuona anafaa kushika wadhida huo kati ya wale waliokuwa wanagombea.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo tarehe 2 Aprili 2019, wakati akituhutubia mkutano wa hadhara mjini Mabarali akiwa kwenye mwendelezo wake wa ziara ya siku nane.

Akihutubia kwenye mkutano huo, Rais Magufuli amesema hakustahili kuwa rais, bali wananchi wa Tanzania walikuwa na sababu za msingi za kumchagua.

Na kwamba, Watanzania waliamua kumchagua kwa kuwa, waliamini anaweza kutatua matatizo yao hasa ya wanyonge.

“Mlinichagua kuwa kiongozi wenu, sikustahili kuwa Rais, mliamua kuwa Magufuli tunampa urais. Sasa tuna miaka mitatu kwenye uongozi na tuliahidi kutekeleza Ilani ya CCM, mawaziri wameeleza tuliyofanya na ambayo bado hayajafanyika wameeleza changamoto zake,” amesema Rais Magufuli.

error: Content is protected !!