January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Magufuli atakiwa kufuata ya Mwl. Nyerere

Spread the love

SHIRIKISHO la Mchezo wa Bao Tanzania, (Shimbata) umemtaka Rais Mteule, Dk. John Magufuli kuvaa viatu vya hayati Mwalimu Julius Nyerere kukuza na kuendeleza michezo ya jadi. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Hayo yameelezwa katika taarifa ya kumpongeza mshindi huyo wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Serikali ya Awamu ya Tano aliyegombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika taarifa hiyo ya pongezi Rais wa Shimbata, Monday Likwepa amesema mchezo wa bao ni mchezo wa amani uliosaidia kuung’oa utawala wa kikoloni na kisultani ikiwa kama moja wapo ya kukutana na kupanga mikakati ya kupambana na ubeberu.

Likwepa amesema pamoja na Mwl. Nyerere kuwa na upenzi wa michezo yote pamoja na michezo ya jadi, yeye binafsi alikuwa anapenda mchezo wa bao.

“Hayati Mwalimu Nyerere alitoa vikombe na kuanzisha mashindano yaliyojulikana kama Operesheni futa madeni (Ofuma)” amesema Likwepa.

Imemtaka pia rais huyo mteule kurejea matamko na msisitizo wa Mwl. Nyerere katika kukuza na kudumisha utamaduni wa Taifa la Tanzania ikiwemo ile aliyosema katika moja ya mikutano yake kuwa “Taifa ambalo halina utamaduni wake ni sawa na nchi isiyokuwa na mwelekeo. Utamaduni nikioo na moyo wa Taifa lolote.”

error: Content is protected !!