April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

DK. Lwaitama amzungumzia Maalim Seif

Dk. Azaveli Lwaitama

Spread the love

UAMUZI  wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad wa kuhamia Chama cha ACT-Wazalendo umetajwa kuwa ni ushujaa. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Msomi na Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha JOKUCO, Dk. Azaveli Lwaitama akizungumza na MwanaHALISI ONLINE amesema, Maalim Seif amefanya uamuzi wenye ukomavu wa kisaisa.

“Hii inakuonesha Maalim Seif ni mtu mweye akili nyingi, wakati ule wa kesi alisema endapo haki isipotendwa upande wake, atachukua uamuzi mgumu.

“Walifikiri ataingia barabarani weee! wale wameishajiuliza mambo ya barabarani yatasaidia nini? Wamejielekeza kwenye ShushaTangaPandishaTanga, Safari Iendelee” amesema Dk. Lwaitama na kuongeza;

“Kwa hiyo, hapo ACT-Wazalendo ni mahala salama kwa Maalim Seif kuendelea na harakati zake kuwasaidia watu wa Zanzibar.”

Amesema kuwa, Maalim Seif anamshikamano na watu wa Zanzibar ambapo wafuasi wake wameitikia wito wake kwa kwenda ACT-Wazalendo “hii inaonesha namna gani kiongozi huyu anaishi kwenye mioyo ya wafuasi wake.”

Jana terehe 18 Machi 2019 Maalim Seif na waliokuwa viongozi waandamizi wa CUF walikabidhiwa kadi ya chama hicho jana terehe 19 Machi baada ya kutambulishwa.

error: Content is protected !!