August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Lwaitama amshangaa Rais Magufuli

Spread the love

Dk. Azaveli Lwaitama, mchambuzi wa masuala ya siasa nchini, ameeleza kushangazwa na kauli ya Rais John Magufuli kutaka kuifanya Ikulu ya Jijini Dar es Salaam kuwa jumba la makumbusho, anaandika Pendo Omary.

Wiki liyopita Rais Magufuli alitangaza azima ya kuingeuza Ikulu ya Magogoni kuwa, jumba la makumbusho ikiwa ni hatua ya serikali kuhamishia ofisi zake kuu mjini Dodoma kabla ya mwaka 2020.

Akizungumza na MwanaHALISI Online leo Dk. Lwaitama amesema “wazo la kuhamisha shughuli za Ikulu ni nzuri.

“…ila kuigeuza Ikulu kuwa makumbusho, haya sio maamuzi mazuri. Hata kama Makao Makuu ya Ikulu yatakuwa Dodoma, ikumbukwe kila mkoa kuna Ikulu ya rais hivyo ni  busara makazi hayo yakabaki kama ofisi za serikali kwa baadhi ya vitengo.

“… mfano, usalama wa taifa na baadhi ya watendaji wa Ikulu. Kwa sababu ukweli ni kwamba, sio wafanyakazi wote wataenda Dodoma,” amesema Dk. Lwaitama.

 

error: Content is protected !!